Social Icons

Saturday, 25 August 2012

Angalizo Tafadhari tazama Picha hizi: Unapo kwenda kula Hotelini, Mgahawa, au sehemu yoyote umewahi jiuliza Chakula kinapo tokea? Tazama Aibu hii ya uchafu kisha chukua hatua!!

 Ukiliangalia Friji kwa Nje ni safi sana kama pale unapo keti na kungojea Chakula kifike, nilipo ona ivyo nilipata kungoja kuona mtu afungue nione ndani kukoje.


 Na Hiki ndicho nilicho kiona, kwa kweli Friji kwanza lilikuwa linanukaaa balaa, pili kulikuwa tayari vitu vinaoza, Na muda mchache uliopita kuna mtu mmoja alitoka kuchukua, Cha kumpikia mteja.
 Hebu tazama Mauchafu hapo Damu zimevia mpaka zimeoza na kuwa sugu, Lakini mnalishwa misosi bado. Hebu cheki hili ni eneo la kuwekea Mayai Lakini kwa jinsi linavyo nuka na chafu  huwezi tamani, Lakini mnarishwa misosi toka humu.


Ndugu zangu Tafakari kabla hauja amua huko unapo kwenda kula hasa wafanyakazi na wanafunzi.. pamoja na wasafiri.... Share ujumbe huu na wenzako

No comments: