Social Icons

Monday, 24 September 2012

HIVI NDIVYO SERENGETI FIESTA 2012 ILIVYO WASHA MOTO NDANI YA UWANJA WA SAMORA IRINGA..


 Msanii wa filamu pia ni muigizaji wa filamu,Shilole akiserebuka jukwaani.
Aunt Ezekiel nae hakuwa nyuma kuachia mbwembwe zake kama kwa
Mkali wa hip hop ndani ya Bongofleva,Roma Mkatoliki akiwarusha vilivyo wakazi wa mji wa Iringa waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta usiku huu ndani  ya uwanja wa Samora.
Ilikuwa ni ya kuvutia sana usiku huu ndani ya uwanja wa Samora,pale wasanii wa THT,Amin na Linah walipopanda jukwaani na kulishambulia vilivyo bila hiyana jukwaa la Serengeti Fiesta 2012,wasanii hao ambao ilielezwa kuwa walikuwa wapenzi baadaye ikadaiwa wameachana kila mmoja akawa anakamua muziki kivya.
Anaitwa Linah kutoka nyumba ya vipaji,THT,Linah akiimba wimbo wake Yalaiti.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,Amin akiimba jukwaani usiku huu mbele ya umati mkubwa wa watu waliojitokeza usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Mkali wa miondoko laini katika anga ya muziki wa bongofleva,Ben Paul akiimba kwa hisia jukwaani usiku huu mbele ya wakazi kibao wa mji wa Iringa na vitongoji vyake,ndani ya uwanja wa Samora,kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2012.
Sehemu ya wakazi wa Iringa wakishangweka vilivyo usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
 Msanii mwingine chipukizi kutoka THT akiimba kwa hisia jukwaani usiku huu.
Msanii Recho akikamua jukwaani.
Anaitwa Recho kutoka THT,kaiimba wimbo wake wa upepo mbele ya umati wa watu waliojitokeza kwa wingi (hawapo pichani) usiku huu kwenye tamasha la serengeti fiesta linaloendelea hivi sasa kwenye uwanja wa samora mkoani Iringa.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Linex akiiimba kwa hisia jukwaani usiku huu kwenye tamasha la serengeti fiesta 2012
Mmoja wa wasanii chipukizi aliyeibukia kwenye shindano la Serengeti Supa Nyota 2012,kutoka Mkoani Mbeya aitwaye Ney Lee pichani akionesha kipaji chake cha kuimba jukwaani usiku huu kwenye uwanja wa Samora,mkoani Iringa ambako hivi sasa kunarindima tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Sehemu ya wakazi wa Iringa na vitongoji vyake wakishangweka usiku huu kwenye muonekano mpya wa tamasha la serengeti fiesta 2012 ndani ya uwanja wa samora.
Ni mkali mwingine kutoka Morogoro kupitia shindano la Serengeti Supa Nyota 2012,Jo Maker akikamua vilivyo mbele ya wakazi wa mji wa Iringa wanaonelea kuingia hivi sasa ndani ya uwanja wa samora,kutibwirika pamoja na muonekano mpya wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Sehemu ya umati wa watu wanaoendelea kuingia ndani ya uwanja wa Samora kujiachia kwa pamoja ndani ya muonekano mpya wa Serengeti Fiesta 2012.
Ni mkali mwingine kutoka jijini Mwanza kupitia shindano la Serengeti Supa Nyota 2012, Young  KIller akikamua vilivyo mbele ya wakazi wa mji wa Iringa wanaondelea kutinga hivi sasa ndani ya uwanja wa samora,kutibwirika pamoja na muonekano mpya wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012.

No comments: