Katika hali isiyokuwa ya kawaida maiti ya mmoja wa viongozi wa mtandao wa madawa ya kulevya waliokuwa wakitafutwa sana nchini Mexico Heriberto Lazcano aliyeuawa umeibiwa kutoka katika nyumba yalikokuwa yakifanyikia mazishi yake.
Rais wa Mexico Felipe Calderon amelipongeza jeshi kwa operesheni iliyofanikisha kuuawa kwa Lazcano, aliyekuwa mkuu wa kundi la Zetas ambalo limefanya mauaji ya kikatili, katika vita dhidi ya madawa ya kulevya nchini Mexico.
Takriban watu elfu 60 wameshauawa katika mgogoro kati ya makundi mbali mbali ya madawa ya kulevya na polisi tangu Rais Calderon aingie madarakani mwaka 2006.
No comments:
Post a Comment