Mmoja wa watangazaji wa redio ya Choice FM inayomilikiwa na Clouds Media Group,Vanessa Mdee akifanya mahojiano mafupi na Mwanamuzuki wa Kimataifa kutoka nchini Marekani Rick Ross,jioni ya leo ndani ya hotel Hyatt Kilimanjaro Kempiski,jijini Dar Es Salaam,Mwanamuziki huyo alizikonga nyoyo za wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake jana usiku kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,lililofanyika kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni.Pichani shoto ni Mtangazaji wa Clouds FM,Millard Ayo nae akirekodi mahojiano hayo.
Mwanamuzuki wa Kimataifa kutoka nchini Marekani Rick Ross,akifafanua jambo kwa msisitizo jioni ya leo ndani ya hotel Hyatt Kilimanjaro Kempiski,jijini Dar Es Salaam alipokuwa akifanya mahojiano na mmoja wa watangazaji wa redio ya Choice FM inayomilikiwa na Clouds Media Group,Vanessa Mdee.Mwanamuziki huyo jana usiku alizikonga nyoyo za wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,lililofanyika kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni.Pichani shoto ni Mtangazaji wa Clouds FM,Millard Ayo nae akirekodi mahojiano hayo.
Rick Ross akiwa amepozi pamoja na washabiki wake,kulia ni Vanessa Mdee na Feza Kessy.
Rick Rose akishoo love na washabiki wake.
Rick Ross akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga ikiwa ni sehemu ya shukurani kubwa kwa kazi iliyofanywa kupitia tamasha la Serengeti Fiesta 2012,ambalo limefanyika usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Lidaz Club,jijini Dar na kupokelewa vyema na washabiki/wapenzi wa tamasha hilo.
Rick Ross akipeana tano na Millard Ayo mara baada kumaliza mahojiano yake,akiwa tayari kabisa kwa kutimka kwenda unyamani kwake nchini Marekani,kuendeleza mambo mengine ya libeneke la muziki.
No comments:
Post a Comment