Social Icons

Thursday, 24 January 2013

JE MWIGIZAJI WA FILAMU LULU KUACHIWA KESHO? SOMA HAPA


.

Taarifa za uhakika nilizozipata
kwa sasa ni kwamba kuna uwezekano mkubwa mwigizaji Lulu akatoka kwa 
dhamana kesho january 25 2013.
Uhakika wa Lulu kupata dhamana 
ulikua jana jumatano january 23 lakini ikawa imeshindikana kutokana na 
kuahirishwa kwa sababu jaji alipata dharura na pia kiwango cha pesa za 
dhamana kilikua hakijatimia.
Chanzo cha kuaminika 
kilichoongea na mtandao wetu kimesema dhamana ya kumtoa Lulu ambae 
amekua chini ya ulinzi kuanzia April 2012 ni milioni 20 za kitanzania.Lulu amekua akishikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mwigizaji Steven Kanumba,
Chanzo Dj Sek Blog

No comments: