Social Icons

Monday, 28 January 2013

LULU AKIREJEA RUMANDE BAADA YA MSAJILI WA MAHAKAMA KUTOKUWEPO OFISINI LEO KUKAMILISHA TARATIBU ZA DHAMANA YAKE.


 Msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akitoka katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo baada ya Msajili wa Mahakama Kuu kutokuwepo ofisini na hivyo kurudi rumande hadi kesho tarehe 29/1/2013 atakapoletwa kwa ajili ya kutimiza masharti ya dhamana ikiwa ni pamoja na kusalimisha  kwa Msajili wa mahakama hiyo hati ya kusafiria, kutotoka nje ya Dar es Salaam  bila ruhusa ya mahakama, kuripoti kwa msajili kila tarehe 1 ya kila mwezi, kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali  ambao watasaini bondi ya Sh.milioni 20 kila mmoja. Lulu anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba. 
Gari lililomleta Lulu likiondoka mahakamani hapo.
Lulu akisindikizwa na askari Magereza. 
Lulu akipanda katika gari la Magereza kurudi Rumande, baada ya kukamilisha taratibu za dhamana hiyo na kukosekana kwa Msajili wa Mahakama Kuu, mahakamani hapo. 
Picha na Habari Mseto

No comments: