Social Icons

Wednesday, 2 January 2013

Msanii wa Filamu afahamikae kwa jina la Sajuki Afariki Dunia leo


Taarifa iliyotufikia asubuhi hii na kuthibitishwa kutoka katika vyanzo vyetu vya habari, inaeleza kuwa Msanii aliyekuwa akisumbuliwa na Maradhi ya kiafya kwa muda mrefu,afahamikae kwa jina la Sadick Juma Kilowoko Maarufu kwa Jina la Kisanii SAJUKI Amefariki Dunia mapema leo asubuhi.

SAJUKI ambaye hivi karibuni Serikali ilijitolea kubeba jukumu la kugharamia matibabu yake na hatimaye hivi karibuni kulazwa kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU) kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili,amefariki Dunia mapema leo majira ya saa moja. 

 Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahali pema peponi-Ameni. 

 Wadau tutazidi kutaarifiana kwa habari nyingine kuhusiana na msiba huu kwa kadiri zitakavyokuwa zikipatikana.

No comments: