Social Icons

Friday, 1 February 2013

DK. CHENI...NIMEMALIZA KWA LULU NAHAMIA KWA KAJALA". SOMA HAPA

STAA
aliyekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha msanii wa filamu Elizabeth
Michael ‘Lulu’ anapata dhamana, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ amefunguka 
kuwa baada ya kufanikiwa kwa Lulu sasa anahamia kwa msanii mwingine, 
Kajala Masanja.      Akizungumza

nje ya Mahakama Kuu jijini Dar baada ya Lulu kuachiwa, Dk. Cheni 
alisema kwa sasa anaanza mchakato wa kumsaidia Kajala mpaka ajue hatima 
ya kesi  inayomkabili.

“Unajua Lulu siyo mtu wa kwanza kumsaidia na mama yake ndiye aliniomba, nilishawasaidia wengi. 

Hata
Cloud alipofungwa nilifuatilia mimi na Dude mpaka mwisho, hatukukata 
tamaa na kwa Kajala nitafanya hivyo kwa sababu ni mwenzetu jamani, 
naamini Mungu anaweza sana na atafanikisha kila kitu,” alisema Dk. 
Cheni.

Kajala
anasota Segerea akikabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyokuwa imewekwa 
bondi na serikali kutokana na mumewe kutakatisha fedha haramu.

No comments: