Social Icons

Monday 8 July 2013

HAKIKISHA HUYAFANYI MAKOSA HAYA SABA KWA UNAYE MPENDA KWEA DHATI


KUNA mambo unapaswa kuyaweka mbali sana. Hakikisha hayaingii kwenye mapenzi yako. Kuyafanya, maana yake unakuwa unauchimbia kaburi uhusiano wako mwenyewe.
Tunapenda kuongozwa na fikra zetu. Kila mmoja anataka mwongozo wa maisha yake uendane na halmashauri ya ubongo wake. Hufanya hivyo, bila kujua kuwa kuna kikomo fulani ndani yake. Akili na matakwa ya moyo, wakati mwingine vinaweza kukupoteza.
Moyo unaweza kumpenda mchawi na ukawa huelewi kitu kwa chochote utakachoambiwa. Penzi la jambazi likikuingia, serikali ndiyo utaiona ni katili kwa sababu inamsaka mwenzi wako usiku na mchana. Hii ina maana kuwa mapenzi ni zaidi ya fikra za kila mtu.
Hutokea watu kuachana wakati bado wanapendana. Migogoro midogo inawafanya watengane, matokeo yake kila mmoja anabaki akiumia kivyake.
Huo ni mfano mmoja kati ya mingi inayoonesha kwamba mapenzi yapo juu ya fikra za kawaida. Inahitaji utulivu wenye mashiko ya sayansi ya saikolojia.
Kuna ambao waliishi kwa mategemeo ya kuachana. Wakiamini wamechokana, matokeo yake kwenye ubongo wao wakatengeneza maneno: “Ipo siku.” Hata hivyo, miezi na miaka ikakatika mpaka wakazikana. Kumbe Mungu aliwaandikia wawe pamoja mpaka kifo ila wao hawakujua.
Dosari ya aina hiyo inatokana na wawili wanaopendana lakini upendo wao ukapofushwa na migogoro ya hapa na pale. Nasisitiza kuwa watu ni lazima wagundue mapema matatizo yao kabla ya kuhisi kwamba kati yao hakuna mapenzi. Vilevile, kila mmoja amuelewe mwenzi wake ni binadamu na siyo malaika.
Ana mapenzi naye, tena mapenzi makubwa. Hata hivyo, hiyo haimfanyi awe malaika. Ni binadamu, kwa hiyo wakati anadumisha mapenzi yake, anaweza kufanya makosa mengi. Jaribu kumvumilia kwa sababu ameumbwa na udhaifu, hajakamilika.
Baada ya utangulizi huo, ni vizuri kujua kuwa yapo makosa ambayo wengi huyafanya, tena mara nyingi bila kujua. Tunaishi nayo, matokeo yanakuwa ni mazoea. Hata hivyo, mara nyingi hutokea yanaharibu uhusiano ndiyo maana nimechagua tuyajadili. Yafuatayo ndiyo makosa yenyewe:

KULICHEZEA KAMARI PENZI LAKO NA MAISHA YAKO
Hapo ulipo hujawahi kuona mtu anapambana kuhakikisha mwenzi wake anabadilika tabia? Bila shaka tayari ulishajionea. Je, umejifunza nini kutoka kwao? Ni kweli kabisa kwamba mwenzi wako si malaika, kwa hiyo mnapokutana lazima mtatofautiana, je, ikitokea hamuendani kabisa?
Umejitahidi kumuweka kwenye mstari unaotaka lakini mwenzako haendi. Unasubiri nini? Kung’ang’ania penzi la mtu ambaye huendani naye, ni sawa na kuuchezea kamari moyo wako, vilevile ni sawa na kuyachezea karata tatu maisha yako.
Upo na mwenzi wako ambaye hakutoshelezi. Mnakutana mara nyingi lakini hakufikishi pale unapotaka upelekwe na mwandani wako.
Unanyamaza tu kwa imani kuwa ipo siku ataweza, siku zinakwenda na mabadiliko hayaonekani. Unajipa matumaini kedekede kwamba kuna siku nyoka ataota miguu na jongoo atakuwa na macho.
Chanzo GPL

No comments: