Najua na nakutambua kwamba Eric ni Mshikaji wangu kitambo sana kwa kweli Tangu pande za Nabu City mpaka sasa, tumekuwa tunaishi pamoja vizuri sana, Leo hii Jamaa kapiga hatua mbele ameamua Kukimbia kambi inayo watatiza vijana wengi yani ile ya Ukapera.
Hapa Pichani Kijana Eric akiwa ametwanga usuti wake si wa kawaida akiwa na maiwaifu wake pamoja na wazazi wao
Hakika hili ni tukio la aina yake na la kipekee kabisa .. Harusi hiyo ilikuwa si mchezo maana mbeleni nimewaona rafiki zangu wamewakilisha vilivyo
Eeewaah.... Sasa hapa kulia ni Kijana Erick akiwa na maiwaifu wake kijana anatazama mbele huku mai waifu akitabasamu kwa chat kuashiria ishara ya ushindi...
Mai waifu wa Erick ambao sasa wamepanda cheo na kuitwa MR and MRS Erick akiwa katika picha ya pamoja na wale waliomsindikiza kusherehesha
Mtu mzima Erick akiwa anapata UKODAK wa kumbukumbu na madadaz walio wasindikiza.... eeeh namuona mtu mzima mwengine F. Katata akiwa kwa mbali Kama FBI anamsimamia vema Erick.. dah ilikuwa Tamu sana harusi hii
Basi ndo ilivyo kuwa kwa ufupi Harusi ya Erick picha zaidi tawawekea hapa hapa msikose.... Kwa ujumla mimi Binafsi binafsi yes... Mimi binafsi maana hii si Blog yangu binafsi napenda kuchukua nafasi hii.. Lakini kwa kuungana na Wasomaji wangu wa Nguvu wote kumpa Hongera sana Kijana Erick mtu wangu wa Nguvu sana kama anasoma ananipata poa kwa Kuachana na Ukapera na kuingia katika GAME la Ndoa.. Tunakutakia maisha Mema kaka MUNGU AWE NANYI. MPENDANE DAIAMA KAMA MLIVYO KULA KIAPO KANISANI
KWA NIABA YA WASOMAJI WANGU WOTE NAPENDA KUWASILISHA SALAMU ZETU
MIMI
FREDY TONY A.K.A SAR FRENJE
No comments:
Post a Comment