Social Icons

Friday 23 May 2014

LEO KATIKA MAHUSIANO: HAYA NI MAMBO YENYE THAMANI KWENYE MAPENZI! SOMA HAPA UELIMIKE NA UACHE KULALAMIKA ETI HAUPENDWI.


KUNA watu ambao huwa wanaumiza kichwa kuhusu mambo ya kuwafanyia wenzi wao ambayo yana thamani kubwa. Kwa bahati mbaya sana ni kwamba wengi huwaza kuhusu fedha na mali.

Rafiki zangu, yapo mambo ambayo yanaweza kuonekana ya kawaida tu au si ya lazima sana lakini kumbe yana uzito na thamani kubwa sana kwenye uhusiano.

Wengi wakitaka kufanya jambo la kumfurahisha mpenzi wake, huwaza katika ukubwa. Hufikiri kuhusu outing, mavazi ya gharama, vito vya thamani n.k.

Wapo wanaofikiri labda kwa kutoka na mwezi wake kwenda naye kwenye hoteli kubwa ya kifahari ya nyota tano na kulala kwa usiku mmoja lina thamani kubwa.

Pengine wapo wanaofikiri kuwa kuwanunulia wenzi wao vitu vya thamani kubwa kama cheni ya dhahabu, gari nk ndivyo vyenye thamani pekee!

Si kweli. Ni ukweli usio na shaka kwamba, mwanamke anapenda kufanyiwa vitu vyenye thamani na mwanaume wake. Ukweli unabaki kuwa, wakati mwingine unaweza kuwa unatamani kumfanya mwenzi wako awe na furaha muda wote lakini mfuko wako ukawa hauruhusu!

Hulka ya wanawake wengi ni kutamani kuona mwenzi wake anamuona mtu muhimu na anakuwa naye karibu muda wote. Wanawake hawajali sana vitu vya thamani kama wanaume wanavyofikiri.

Kumkumbatia mwanamke na kumbusu katikati ya midomo yake, ukisindikiza na maneno matamu ni zaidi ya gari utakalomnunulia – kikubwa hapa, mwanamke huyo awe kweli ana upendo nawe na si kuwa yupo kibiashara!

Katika mada hii, nimekuandalia vitu vichache ambavyo kwa hakika, kwa mujibu wa utafiti nilioufanya, ni vitu muhimu kwa wanawake. Ukifanya vyote au sehemu yake, unamfanya mwanamke wako ajihisi yupo katika mikono salama.

Bado thamani ya mali na vitu vingine vitabaki katika uhalisia wake, lakini kwa hakika mambo yafuatayo hapa chini, huwachanganya sana wanawake.

KADI YA MAHABA
Ni utaratibu uliozoeleka sana kipindi cha nyuma kidogo. Sasa hivi teknolojia imebadilika, kadi inaweza kupatikana hata kwenye mitandao mbalimbali ya internet.
Hata hivyo, bado inaonekana kuwa mwanamke anapenda na anatamani kuona mwanaume wake anamkumbuka kwa kumtumia kadi.

Wanaume wengi ni wavivu, lakini kwa sababu ya ustawi wa penzi lako, jaribu hili. Nunua kadi yako yenye ujumbe mzuri, andika maneno mengine kwa mkono wako mwenyewe, pulizia manukato unayotumia, kisha mtumie / mpelekee mpenzi wako. Utakuwa umemroga!

NYIMBO, MASHAIRI
Wanawake wanapenda sana kufahamu kuwa kweli alipo anapendwa. Nyimbo nzuri za mapenzi ambazo zitaeleza uzuri wake na namna unavyompenda na kumthamini, vinazidi kukuweka katika kilele cha umiliki uliotukuka.

Mchagulie mpenzi wako wimbo redioni, taja jina lake, lako na ujumbe wako. Utamfanya ajisikie fahari sana. Mashairi katika magazeti mbalimbali na majarida pia huongeza ladha ya mapenzi.

Anachojali mwanamke ni ile hali ya kuona kuwa, unampenda na unaweza kuthibitisha hilo hata mbele ya watu wengine. Kusikia akitajwa redioni au ameandikwa gazetini ukionyesha hisia zako za kumpenda, kutamchanganya na kumfunga kabisa hisia za kufikiri kukusaliti.

atizo wanaume wengi hawatilii maanani haya mambo lakini kama unataka kuwa dume la mbegu kwa mwanamke wako, jaribu uchawi huu.
Wiki ijayo nitakuwa hapa katika sehemu ya mwisho,

USIKOSE!Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Saikolojia ya Uhusiano anayeandikia Magazeti ya Global Publishers. Kwa sasa anaandaa kitabu chake kipya cha Maisha ya Ndoa.
GPL

No comments: