Social Icons

Tuesday, 10 June 2014

HAPI BATHDEI BESTE YANGU MWANADADA !

Mara nyingi sana kila mmoja wetu huwa na shauku sana ya kuingoja Tarehe pamoja na Mwezi ambao alizaliwa kwa wenzetu wazungu wanaita Birthday na wanapotaka kukupa pongezi wao husema Happy Birthday ni neno ambalo sote tunalifahamu. Lakini kwetu sisi kibongo bongo na Kiswahili Chetu au Kiswanglish Tunasema Tuu Heri ya Kumbukumbu yako ya kuzaliwa ama Hapi Bathidei..

Hivyo hivyo leo ni siku muhimu sana ya kwa Rafiki yangu, Dada yangu, Mtu wangu wa Karibu sana katika maswala ya kazi zetu mbalimbali si Mwengine ni huyu hapa Pichani chini hapo ambaye naye leo anatimiza Miaka Kadhaa na kuikumbuka ile Tarehe na Mwezi alio zaliwa ingawa leo Miaka mingi imepita mpaka anasherekea tena.

Ni Mtu ambaye kwa ukweli kama nilivyosema binafsi napenda sana kazi zake binafsi anazozifanya kupitia Blog yake ama kwa Lugha ingine Libeneke la Mwanadada Blog ambapo na wewe ukitaka kujiridhisha na kuona Ingia hapa www.mwanadada.blogspot.com na utajionea wewe mwenyewe kwa jinsi gani alivyo Mbunifu katika mtandao wake ambao kwa uhakika naweza sema haufanani na hiyo mengine yeye amaweka tofauti kabisa.
Basi Kupitia Mtandao huu, napenda kuungana kwanza na wasomaji wangu wote pili na watu wote ambao wanamfahamu mwanadada kwa urafiki, ama undugu kumtakia Sikukuu njema ya kukumbuka siku yake ya Kuzaliwa na pia Binafsi nakutakia miaka mingi zaidi, Uchape kazi zaidi ubunifu wako uongezeke mara Miliioni zaidi na zaidi na zaidi uwe na Afya njema.

Happy Birthday

Mwisho: Tunaomba Location ya kuja kukata Kekiii


No comments: