Social Icons

Monday, 24 November 2014

LEO KATIKA MAHUSIANO: SHOGA USITOE SIRI ZA MUMEO UKAZANI NDIO SIFA NJE UTAACHWA! SOMA HAPA SIO UNAKUWA MSHAMBA TUU



Ni siku nyingine ya Jumanne ambapo tunakutana katika safu yetu hii mahususi kwa kuelimishana na kukosoana kwa lengo la kuboresha uhusiano wa kimapenzi na wenza wetu.

Baada ya wiki iliyopita kuzungumza nanyi kuhusu madhara ya kuchunguza simu ya mume, leo nataka kuzungumzia ‘topiki’ kuhusiana na wanawake wanaopenda kutoa siri za wapenzi au waume zao nje.
Nimeamua kuzungumzia ishu hiyo kwa sababu nimeshuhudia mara kadhaa wanawake wakiachwa, kisa kikiwa kuwaeleza wenzao mambo yao ya ndani.

Tabia hiyo imeshamiri sana siku hizi ambapo wanawake hutoa siri za waume zao wakifikiri watasifiwa na wenzao kumbe wanajiharibia.Utamsikia mwanamke aliye kwenye ndoa akiwaambia wenzake jinsi mumewe alivyo goigoi wakati wa makesheshe jambo litakalowafanya wenzake kumbeza mumewe kwamba ni mwanaume suruali nk.

“Jamani mnamuona mume wa Khadija alivyopendeza? Lakini huwezi amini kwenye yale mambo yetu hawezi kitu,” mmoja wa shoga zako atawaambia rafiki zake baada ya kumuona mumeo akirejea kutoka kazini, chanzo ni wewe kutoa siri hiyo nje.

Wengine, ili waonekane wameolewa na wanaume waliojaaliwa utundu na mambo mengi ‘uwanjani’, huwasifia kwa wenzao namna wanavyofurahia mapenzi pasipo kujua kama wanawapa mwanya wa kuwaibia penzi lao.

Utamsikia mwanamke ambaye mumewe ni mtu wa dili akiwaambia wenzake kwamba mumewe kaporomosha bonge la mjengo huko Mbezi Beach, kanunua Coaster au benzi mbili na kufungua miradi kibao.

Hivi shoga yangu unafikiri mumeo akijua unavyovujisha siri zake atakuacha, ni wazi atakupiga chini kwa sababu atabaini unaweza kusababisha aanze kuchunguzwa anakozipata fedha kisha kukamatwa na kuishia gerezani.

Shoga yangu, mwanamke unatakiwa kuwa msiri wa mambo yote unayofanya na mumeo hata kama jamaa ana tatizo la kukojoa kitandani mfichie siri hiyo.Hebu fikiria siku akigundua siri kuhusiana na tatizo lake la kukojoa kitandani au kukoroma kama mlevi wa gongo akilala usiku umewaambia wenzako, patakalika kweli?

Naamini hakuna mwanaume anayeweza kuvumilia upuuzi huo, ni wazi atakutimua na nafasi yako itachukuliwa na mwenzako anayejua kutunza siri za ndani.

Tuonane wiki ijayo kwa mada nyingine.

NA GLOBAL PUBLISHERS

No comments: