Kwa wale nitakaowakwaza naomba mniwie radhi lakini kweli hata mimi
hainipendezi kuyasema haya ila ni vema tu niwaeleze dada zangu kwasababu
ukweli unaoumiza ni bora, kuliko uongo unaofurahisha.
Hakuna mwanaume riijali anayeweza kuwa na mwanamke mmoja, eidha awe
ameoa au hata kama hajaoa. Hakuna mwanaume wa aina hiyo Karne hii,
usijidanganye kukimbilia kwenye ndoa ukiamini kwamba baada ya kuolewa
utajimilikisha huyo mwanaume aliyekuoa, never.
"Mchele mmoja mapishi mbalimbali", utakuta wewe mwanamke kila siku
ukikutana na jamaa yako faragha lazima yeye ndio aombe kamchezo, wakati
kuna sehemu akienda mwanamke mwenzako ndio anaandaa mazingira ya kuomba
kamchezo kutoka kwa jamaa, now u see the difference.
Mara zote mkitoka lazima wewe ndio uwe ume suggest mtoke tena yeye ndio
ana pay bills, wakati kuna mwanamke mwenzio some where ingawa sio mara
zote, ila mara chache chache yeye ndio anamuomba jamaa watoke na ndio
ana pay bills, umeona.
Humshauri jamaa hata kununua an asset, wewe ni kuvaa na kujirusha wkt
kuna mwanamke mwenzako kashatafuta kiwanja kwa siri huku mkononi ana
angalau robo amount ya gharama nzima ya kiwanja, upo hapo.
Kwa mliooana, mumeo karudi Home, hata kabla hujampokea ni makelele
mtindo mmoja, unaleta mere allegations kwamba anakusaliti wakati
hujathibitisha, yani wivu yako tu yanakuwehusha, wakati kuna mwanamke
mwenzio jamaa akienda kwake anapokelewa kwa utulivu, anaenda kuogeshwa
tena kwa maji yenye iliki, anakula chakula tena kile anachokipenda,
anakandwa apunguze uchovu then anapumzishwa, unaona hapo.
Dada zangu yani hakuna mwanaume anayeweza kuwa na mwanamke mmoja sababu
hawezi kuwa na vyote ambavyo wanaume tunavihitaji. Sisemi michepuko
iendelee ila hiyo ndio hali halisi, angalau mjitahidi kuwa mnasoma alama
za nyakati ili angalau apunguze michepuko ila sio aache kabisa.
CHANZO VIJIMAMBO BLOG
No comments:
Post a Comment