Social Icons

Monday, 12 October 2015

BREAKING NEWS: TANZIA: WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA MH. DKT. ABDALLAH KIGODA AMEFARIKI DUNIA LEO NCHINI INDIA

Ikiwa una Tukiko lolote au Habari yoyote usisite kutumia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda enzi ya uhai wake.

Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda amefariki dunia leo saa 10 jioni nchini India alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashilila amethibitisha taarifa hizo, na kusema kuwa Dkt Kigoda alikuwa akitibiwa katika hospitali ya Apollo, New Delhi na kwamba taarifa zaidi zitatolewa baadaye.

Kwa mujibu wa kaka wa marehem Sadiki Kigoda aliyezungumza na EATV siku chache zilizopita, alisema kuwa Dkt Kigoda alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya figo kushindwa kufanya kazi.
.

Endelea fuatilia Taarifa zaidi hapa 

Chanzo: EA TV

No comments: