Social Icons

Friday 23 October 2015

KUTANA NA BLOGGER FREDY NJEJE AKIONESHA KIPAJI CHAKE KATIKA SANAA NA UBUNIFU WA HALI YA JUU


 
 Hapa ni hatua za mwanzo za kupata ni jinsi gani utaweza kuunda Bendera ya Tanzania katika Vitu mbalimbali kama Bangili, Hereni na Mkufu.
 Kazi hii inahitaji umakini mkubwa hasa wakati wa kuziweka Rangi sawa ili upate kile unacho hitaji
Hapa vinazidi kukamilika
Hii ni hatua ya kuendelea kutengeneza vito hivi
Hapa Bangiri imekamilika, pete , hereni na Key Holder vyote vipo sawa lakini bado havijakamilika kwa hatua ya mwisho
Kishikizo cha Funguo kimekamilika hapa Key Holder
Hapa kila kitu kikiwa kimekamilika safi kabisa tayari kwa matumizi , ukitazama utaona kuna Bangili , pete, Key Holder, Kidani na Hereni
Pichani ni Mama Shujaa wa Chakula 2015 akiwa Marekani hivi karibuni, lakini ukitazama amependeza kwa kuvalia Hereni, Mkufu, na pete kwa mbali vyote vikiwa ni kazi ya mikono yangu .

Ilikuwa mwaka 1999 nikiwa kidato cha Tatu mwezi wa kumi na mbili ambapo ilikuwa ni Rikizo ya sikukuu ya Christmas, katika pita pita zangu mitaa ya Sinza Mapambano nilikutana na jamaa flani wawili mmoja akienda kwa jina la Wa Boy na Mwengine Alawi, Hawa jamaa walikuwa wanafanya sanaa na kuuza vitu mbalimbali ambavyo walikuwa wanatengeneza wao wenyewe, ikiwa ni pamoja na Sanamu, Batiki, Miochoro na Shanga.

Katika vyote mimi niliipenda zaidi sanaa ya Shanga kwa kuwa kuchora nilikuwa tayari nafahamu pia kufanya Batiki nilikuwa nafahamu vizuri, hii ya kutunga shanga ndicho kilikuwa kitu sijawahi kifanya, lakini kwa kuwa ndio ilikuwa ni Fursa kwangu pekee nilijitahidi nikawaomba urafiki na nikaanza shinda pale kijiweni.

Kimsingi jamaa walikuwa wapo vizuri sana katika Sanaa hiyo ya utungaji wa Shanga, na kipindi hicho wao kwa kuwa walijua mimi mchoraji basi zikitokea kazi za kwenda kuchora kwenye masaluni, kuandika mabango na vibao mbalimbali walikuwa wakinituma kwenda kufanya shughuli hizo.

Mimi lengo langu lilikuwa ni moja tuu kutaka kujua kutunga shanga, Sasa sikumoja wakati tunapiga piga story nikawadokezea kuwa napenda pia kujua kushona Shanga, Jamaa hawakuwa wachoyo wakakubali lakini kimsingi walinipa mtihani mgumu sana kabla sijaanza wa wao kumwaga shanga mchangani na kunisihi niziokote zote kwa kutumia Mshipi maalum kwa ajili ya kushonea Shanga hizo. Zoezi hilo lilinitoa Jasho sana na baadae nilipolikamilisha ndipo nikafuzu kuanza kushona hizi shanga.

Katika kujifunza Shanga ilinichukua muda kwa sababu kila kitu kina hesabu zake na pia kama hauna kipawa ni ngumu sana kuelewa baadhi ya mambo Mfano mtu anasema kwamba anataka Bendera ya Taifa, wewe unafundishwa tuu Sheria za kushona lakini ili Bendera ya Taifa ya Tanzania itokee hiyo ni akili na ubunifu mkubwa unatakiwa kwa hiyo nilipata changamoto sana lakini baadae nilijua.

Katika kutunga Shanga kitu cha kwanza kabisa mimi kujua ilikuwa ni kutengeneza Bendera ya Jamaica kwa kuwa wateja wengi walikuwa wakitamani kuvaa rangi hizo maarufu kwa Jah People na baadae nikajifunza vitu mbalimbali na kubwa zaidi nikafahamu zaidi ya aina 20 za ushonaji wa shanga kutokana na mahitaji ya watu baadhi ya hivyo ilikuwa ni pamoja na Vidani vya shingoni, Hereni, Mikufu, Bangiri, Viatu, Sendo, kudalizi shati kwa kutumia ushanga, pamoja na vitu mbalimbali. 

Nilipo maliza rikizo na kurudi shule hii ilikuwa ni moja ya Biashara yangu kubwa ambapo mwaka 2000 nilipata tenda kutengeneza vitu mbalimbali na kuuza kwa dazani kwa wafanyabiashara wa urembo soko la  Mwanjelwa kabla halijaungua, katika hivyo nilikuwa nauza dazani moja kwa Tsh 15,000 ambapo nikiuza dazani 20 nilikuwa napata Tsh 300,000 kwa dizaini za kawaida lakini zile dizaini Bora zaidi nilikuwa nauza dazani moja kwa tsh 30,000 ambapo walikuwa wakichukua kuanzia dazani 20 jumla yake inakuja Tsh 600,000 ambapo faida ilikuwa kubwa ingawa wao walikuwa wanapata zaidi. Hapa nilikuwa nauwezo wa kutengeneza dazani ya kawaida kama hereni kwa siku moja , muda mwingi nilitumia kushona shanga hizi. 

Niliendelea na kazii hii ya kutengeneza Shanga mpaka mwaka 2003 ambapo Mwaka 2004 nilikwenda kusoma Chuo ambapo nilisimama kwa muda bila kuendelea na kazi hii kwa sababu nilijua ni Kipaji tuu hakiwezi potea ingawa mwaka 2007 nikiwa nimemaliza Chuo nilianza tena shona shanga ingawa haikuwa kwa biashara lakini kwa mazoezi tuu.

Sasa ni miaka Nane(8) imepita sikuwahi kugusa Shanga mpaka mwaka Huu 2015 ambapo ndipo nimekumbuka kujikumbushia kipaji changu na hii imetokana na baadhi ya watu kuona kazi zangu za sanaa kwenye  ukurasa wangu wa Facebook na kunisihi nianze tena kushona kwa sababu ni pesa,na nisikalie kipaji tuu. Niliwasikiliza  na ndio maana nimeifanya kazi hii ninayo iwasilisha hapa kama kithibitisho cha kuwa bado nipo fiti kwenye kazi hii.

Lengo la Makala hii fupi ni kutaka kuonesha kuwa pamoja na mtu kuwa unafanya kazi mbalimbali lakini ni muhimu kukumbuka kipaji chako maana ni Karama na kipawa toka kwa Mungu, ewe Kijana mwenzangu nakusihi kama unakipaji basi usikiache 

Imaandaliwa na Fredy Anthony 
Wasiliana nami kupitia Whatsapp +255765056399 au nipigie kupitia 0654221465


No comments: