Social Icons

Thursday 15 October 2015

RAIS JAKAYA KIKWETE KUWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA BANDARI YA BAGAMOYO

Ikiwa una Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo au Habari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe  akizungumza na waandi wa habari wapo picha juu ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo utakaokuwa wa aina yake Afrika Mashariki na Kati, unatarajiwa kugharimu dola za Marekani bilioni 10 na kukamilika kati ya miaka mitano hadi saba ijayo. kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa CMHI ambaye pia ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni ya China Merchant Group Dk Hu Jianhua.kikao hichi kimefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akizungumza juu ya ujenzi huo na  Mjumbe kutoka China Mkurugenzi Mtendaji wa CMHI ambaye pia ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni ya China Merchant Group Dk Hu Jianhua.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akiagana na  Mjumbe kutoka China Mkurugenzi Mtendaji wa CMHI ambaye pia ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni ya China Merchant Group Dk Hu Jianhua.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbarimbari na Mjumbe kutoka China Mkurugenzi Mtendaji wa CMHI ambaye pia ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni ya China Merchant Group Dk Hu Jianhua.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)


 WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe amewathibitishia wakazi wa Bagamoyo kuwa wale wote watakaoguswa na mradi wa ujenzi wa bandari mpya watalipwa fidia na wengine watajengewa nyumba kwenye maeneo ya mji huo.

Akizungumza na wandishi wa habari badaa ya kukutana na Mkurugenzi wa Kampuni ya China Merchants Group itakayosimamia ujenzi huo, Dk Hu Jianhao, Membe alisema katika ujenzi huo utakaochukua hekta 2400, wananchi wote watakaohuswa hawataachwa bure.


“Mradi huo ni mkubwa sana unaoshirikisha kampuni hii ya China Merchants Group, wawekezaji kutoka Oman ambao wataalamu wao pia wameshafika na Serikali ya Tanzania. Tunatarajia kuwa utaibadilisha Bagamoyo kwa kiasi kikubwa na kuufannya kuwa mji wa viwanda, hatua itakayovuta wawekezaji wengi zaidi na kuzalisha ajira nyingi,” alisema.

Mradi mzima wa ujenzi utajumuisha eneo hekta 800 kwa ajili ya ujenzi wa bandari na eneo la hekta 1,700 kwa ajili ya ukanda wa viwanda.

Mazungumzo hayo ni sehemu ya awali ya maandalizi kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa bandari hiyo, katika sherehe inayotarajiwa kuongozwana Rais Jakaya Kikwete leo.

Mradi huo wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo utakaokuwa wa aina yake Afrika Mashariki na Kati, unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani bilioni 10 na kukamilika kati ya miaka mitano hadi saba ijayo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Dk Florens Turuka jana, Rais Kikwete ataweka jiwe hilo la msingi kwa ajili ya uzinduzi wa awamu ya kwanza ya mradi huo.

Eneo hilo  litaendelezwa chini ya makubaliano ya Serikali ya Tanzania, Kampuni ya China ya Merchants Holdings International (CMHI) na Mfuko wa Taifa wa Dharura wa Oman (SGRF).

Chini ya ushirikiano huo, Serikali inawakilishwa na Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA) na Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA), Oman itawakilishwa na SGRF na China CMHI.

Dk Turuka alisema mradi huo pia utahusisha ujenzi wa miundombinu kama vile reli, mitandao ya barabara, umeme, umeme, gesi na mitandao ya mawasiliano.

Mradi huo unatarajiwa kuibadili Tanzania na kuwa kituo kikuu cha usafirishaji kwa wafanyabiashara wa ndani na wa kimataifa ambao wataunganishwa na viwanda vitakavyozalisha bidhaa zilizoongezewa ubora.

Kwa mujibu wa Dk Turuka, wazo la kuwepo mradi huo, limetokana na uhusiano wa muda mrefu wa kidiplomasia baina ya Tanzania, China na Oman katika kuhamasisha uimarishaji wa viwanda Afrika jambo litakalosaidia kuongeza ajira nchini.
mwaka 2008, Rais Kikwete alipotembelea China na kuzungumza na Rais wa nchi hiyo, Hu Jintao, na kuafikiana kujenga bandari hiyo.

Sherehe za kuweka jiwe la msingi zitahudhuriwa na wageni wa kimataifa na wa ndani wakiwemo wawekezaji katika mradi huo.
Wengine wanoatarajiwa kuhudhuria ni wanadiplomasia na ujumbe kutoka kwa Sultani wa Oman utakaoongozwa na Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano nchini humo, Shehe Abdullah Al Saadi.

No comments: