Ikiwa una Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo au Habari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com.
Kuna mambo mengi
ambayo kwa upeo wa kawaida unaweza ukaona kuwa mwanaume fulani anakupenda kwa
dhati au anakutamani japo kuwa mambo haya kwa kizazi cha sasa yanahitaji akili
sana kujua kwa kuwa vigezo vilivyokuwa vikitumiwa na wapenzi wa kizamani siyo
kama vya sasa.
Kwa mfano zamani
kupima kama mwanaume ana mapenzi ya dhati, mwanamke atampa sharti mwanaume kuwa
wasifanye mapenzi mpaka waoane na kweli kidume kinaweza kikasubiri mwaka mzima
wakaishia kupiga stori tu.
Kwa siku hizi hali
imekuwa tofauti pengine kutokana na utandawazi na usaliti uliokithiri kiasi
kwamba ukimwambia mwanaume eti msifanye mapenzi mpaka muoane, mwenzako ataona
unamchelewesha japo anaweza akakukubalia usoni lakini moyoni atatafuta mchepuko
na kupoozea hamu ingawa kweli anaweza akawa anakupenda kweli lakini uzalendo
utamshinda atakuwa anakuzuga tu kama anakusubiri siku ya siku kama ugonjwa
utaupata tu humohumo ndani ya ndoa.
Wanaume wengine
wanafanya hivyo kwa kuwa wanajua wapo wadada kibao ambao wakiona mwanaume
ameonesha kamsimamo kakutaka kuwaoa basi ndiyo anajifanya anamkazia mwanaume
huyo kuhusu suala la mapenzi huku kwa wanaume wengine akichepuka kirahisi;
mifano ipo kibao.
Wanaume na wanawake
wa sasa wameshtuka mtu akiwa na mtuye anataka amdhibiti kiasi cha kumtimizia
kila kitu anachokitaka kiasi kwamba asiweze kusaliti, na ndiyo hali halisi
ilivyo.
Sasa katika hali kama
hiyo kumjua mtu yupi anakupenda kwa dhati au anakutamani kabla hamjafikia hatua
ya kufanya mapenzi ukajutia baada ya kujua ukweli wake inabidi uangalie vitu
vidogovidogo tu bila kujali mtazamo wake kuhusu suala la mapenzi.
Swali la kujiuliza
hapa ni moja tu:
-Je, uhusiano wenu
anauweka wazi au ni wa siri?
Ukiona anakwambia
‘ooh mapenzi yetu sitaki mtu ajue, tufanye siri’ hata marafiki zake hataki
wajue kimbia huyo mwongo anakutamani japo sikatai kuwa wapo wengine wanaweza
wakakuweka mpaka kwenye mitandao ya kijamii lakini baadaye wakaja kuwa wasaliti
lakini kosa linaweza likawa lako wewe mwenyewe bila kujua.
Kosa gani hilo?
Kutana nami kesho katika mada inayosema MAKOSA YANAYOVUNJA PENZI LAKO BILA
KUJUA.
Imeandaliwa na Fredy Njeje Blog
No comments:
Post a Comment