Ikiwa una Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo au Habari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com.
[Unguja-ZANZIBAR]
Mwanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF) imeelezwa
kuwa amenusurika katika ajali ya gari iliyotokea mchana wa leo Novemba
Mosi, eneo la kijiji cha Kibele, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja
kwa kile kilichoelezwa kuwa ni mwendo kasi wa gari hiyo.
Kwa
mujibu wa shuhuda wa taarifa ya tukio hilo: “ Ajali imetokea mchana huu
kwenye saa 8.10 ambayo imemhusisha askari wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (TPDF) (jina halikupatikana). Mazingira ya ajali
hiyo ambayo imetokea katika kijiji cha Kibele, Wilaya ya Kati Mkoa wa
Kusini Unguja ni mwendo kasi wa dereva huyo ambaye alishindwa kuidhibiti
gari ndogo aina ya Toyota Spacio yenye namba za usajili Z 511 FG na
hatimaye kuacha barabara na kugonga mnazi.
Baada
ya kugonga mnazi huo, uliangukia gari na baadae gari kuwaka moto.
Dereva alitolewa ndani ya gari akiwa amebanwa na air bags zilizofyatuka
na kuokoa uhai wake. Alipata majeraha madogo ya kuchubuka kwenye mikono
yake iliyokuwa inavuja damu.
Chanzo: Habari za Jamii Blog
No comments:
Post a Comment