Social Icons

Monday, 18 January 2016

HOT: MH. SIMBACHAWENE ASIMAMISHA KAZI WAKURUGENZI KATAVI NA KIGOMA

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @officialfredynjejeblog Twitter @Fredynjeje
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa George Simbachawene

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa George Simbachawene amewasimamisha kazi wakurugenzi katika Mikoa ya Kigoma na Katavi kwa ubadhirifu wa mali za umma.

Waliosimamishwa kazi ni pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi  Bwn. Sulemani Lukanga kwa tuhuma za kununua gari hewa la kubebea takataka kwa kiasi cha shilingi 92,750,000  na  ubadhirifu wa fedha za ujenzi wa skimu ya umwagiliaji ya Kakese kiasi cha shilingi miambili tisini na nne 294,000,000/=na .
kinyume kabisa na sheria za utawala bora.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Eng. Boniface Nyambele anaetuhumiwa kwa uuzaji wa nyumba za serikali bila kufuata sheria za uuzwaji wa mali za umma.

 Mheshimiwa Waziri wa Nchi ameagiza nafasi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma ikaimiwe na Mhandisi Sultan Imari Ndilowa ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maji, Manispaa ya Kigoma, nafasi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda ikaimiwe na Ndugu Lauteri John Kanoni ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi.

Mheshimiwa Waziri wa Nchi, amewataka Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kote Nchini kuwa makini katika kutekeleza majukumu yao wafuate Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo. Serikali haitasita kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wote ambao watakiuka matakwa ya Sheria, Kanuni na Taratibu na kutoweka mbele maslahi ya Umma.

Hatua ya Waziri Simba chawene imefuatia ziara ya hivi karibuni ya waziri mkuu Kassim Majaliwa ambaye alibaini matumizi mabaya ya madaraka na kuhitaji ripoti kamili juu ya ubadhirifu uliofanywa na wakurugenzi hao.


NA BLOGS ZA MIKOA

No comments: