Social Icons

Thursday, 21 January 2016

Lengo langu kubwa ni kusaidia yatima-Prince Haji

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @officialfredynjejeblog Twitter @Fredynjeje

 Prince Haji

Mwanamuziki wa muziki wa Bongo fleva nchini  Haji Juma a.k.a Prince Haji  ameeleza dhamira yake ya kufanya muziki kuwa ni kusaidia Watoto yatima.

Prince ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani katika jimbo la Manchester new Hampshire akifanya vizuri na kundi la Afro Band amesema yupo Marekani kimuziki lakini amepanga kuanzisha bendi mwezi wa sita mkoani Kigoma ikiwa ni pamoja na kusaidia watoto yatima.

''Nimeanza muziki miaka miwili ilio pita niya na madhumuni yangu mimi kufanya muziki  nikiwa na lengo kubwa la kusaidia watoto yatima ''Amebainisha Prince Haji.

Kwa sasa Mwanamuziki huyo ameachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ''kupenda'' wimbo ambao unaakisi maisha yake na mkewe jinsi mkewe alivyomuahidi kumlea  na video yake anatarajia kuitoa jumamosi 30/01/2016.

No comments: