Social Icons

Sunday, 31 January 2016

Mmiliki Wa Mjengwablog Ashiriki Na Kumaliza Half Marathon Ya ' Hapa Kazi Tu' Dodoma..

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @officialfredynjejeblog Twitter @Fredynjeje


Nikiwa kama mmiliki na mhariri wa mtandao wa mjengwablog.com,  Jumamosi ya Januari 31, nilipambana hadi mita 100 za Mwisho kwenye Uwanja wa Jamhuri ili 
kukamilisha kilomita 21.1. Milima ya kwetu Iringa iliniweka kwenye form nzuri kuikabili tambarare ya Dodoma.
Pichani nikimalizia mita 100 za mwisho.
 
Najipanga sasa kuukabili Mlima Kilimanjaro mwezi Juni mwaka huu. Nataka kuhamasisha Watanzania wa Nyumbani Na Diaspora kuutangaza mlima huu mrefu kuliko yote Afrika sambamba na kuutetea theluji yake isije ikayeyuka kutokana na Mabadiliko ya Tabia Nchi ikiwamo uharibifu wa mazingira yanayouzunguka mlima huo.
Kuwepo na matumaini ya uhai wa Kilimanjaro. Soma makala yangu iliyochapwa kwenye # Africablogging kuhusu Kilimanjaro...http://www.africablogging.org/tanzania-there-is-still-hope-for-kilimanjaro/

Maggid

No comments: