Social Icons

Thursday 21 January 2016

Mwalimu Mwislamu aliyewatetea Wakristo afariki Kenya

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @officialfredynjejeblog Twitter @Fredynjej

  Sala Farah alikuwa mmoja wa abiria waliokaidi agizo la al shabab

Mwalimu raia wa Kenya ambaye alisifiwa na kuitwa shujaa wakati Waislamu waliwakinga abiria Wakiristo wakati wa shambulizi la al-Shabab kwenye basi moja kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, ameaga dunia wakati akifanyiwa upasuaji kutibu majeraha yake.

Salah Farah ambaye alikuwa naibu mwalimu mkuu katika shule moja ya msingi mjini Mandera, alipigwa risasi wakati yeye na wenzake walipokataa agizo la wanamgambo wa Kiislamu waliowataka abiria kugawanyika kwa makundi mawili ya Waislamu na Wakristo.
 
Image caption al Shabab wamekuwa wakiendesha mashambulizi nchini Kenya
Ujasiri wa abiria Waislamu ambao walikaidi agizo la wanamgambo la kuwataka wajitenge la sivyo wauawe wote ulisambaa kote duniani wakati habari kuhusu shambulizi hilo ziliporipotiwa tarehe 21 mwezi Disemba.
Mwili wa bwana Farah umesafiriswa kwenda mji wa Mandera tayari kwa mazishi.

BBC Swahili

No comments: