Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @officialfredynjejeblog Twitter @Fredynjeje
Na Fredy Njeje Blog
Ni ngumu kueleza lakini kadili ya uwezo wangu nitawaambia ukweli , hii ni historia yangu ya ukweli kabisa. kwa muda mrefu sana tangu nimeolewa na mume wangu amekuwa hatukubahatika kupata hata mtoto wa kusingizia, tumekwenda kila Hospitali kubwa na ndogo kutazama nani mwenye tatizo tunakuta majibu yale yale, kuwa waganga wanasema sisi sote tupo sawa na tunaweza kupata mtoto, swali likaja kwa nini mtoto haji?
Niliolewa na Mume wangu mpenzi wakati nikiwa na umri wa miaka 18, Mume wangu anaitwa Joshua, ni mume ambaye anayatambua majukumu yake kama baba wa familia ananijali, ananifanyia kila kitu kama Magari kaninunulia mazuri,kama nyumba kajenga mpaka kijijini kwetu,kila kitu ananipa kifupi mimi sina shida za maisha.
Miaka miwili iliyopita kuna rafiki yangu ambaye nilikuwa naye tangu tukiwa watoto alinishauri kitu cha kufanya...lakini nilipuuzia.. katika nyumba nayo kaa na mume wangu kulikuwa na kijana mmoja ambaye alikuwa anasaidia kazi mbalimbali za ndani alikuwa anaitwa Benard mwenye umri wa miaka 22, Tumeishi na huyu kijana tangu akiwa na umri wa miaka 8, tunamjali na kuishi nae kama mtoto wetu wa kumzaa.
Miezi kadhaa baadae Mume wangu alisafiri kwenda kwenye biashara zake, huu ulikuwa ni muda muafaka wa mimi kuongea na Benard kuhusiana na maisha yangu mpaka mambo yangu ya ndani kabisa kwa kuwa nilikuwa huru sana kuyasema hayo.
Mazungumzo haya yalikuwa yanafanyikia chumbani kwa mume wangu, baadae mazungumzo yalipopamba moto nilifunga na mrango kwa funguo na kuzitoa mlangoni, ghafla niliacha mazungumzo na kumuomba Benard tufanye mapenzi, jamaa akakataa kufanya mapenzi nami, alipozidi kukataa nikamwambia kuwa tamfukuza aende kijijini kwao, na kwa kuwa alikuwa anajua kijijini ni shida alikubali kufanya mapenzi nami, tulifanya mapenzi mara tano kabla siku haijaisha.
Siku iliyofata Mume wangu alirejea kutoka safari , na siku 13 baadae nikagundua kuwa mimi ni mjamzito bila kumwambia Benard kuwa nilikuwa mjamzito,nilichofanya nilimpatia Tsh Mil2 pesa tasrim ili arejee zake kijijini.. Lilivyokuwa jinga likachukua zile pesa kwa furaha kisha akasepa.
Baada ya hapo ilibidi nimwambie mume wangu kuwa mimi ni mjamzito , ghafla mumewangu alibadilika na kuwa mtu mwenye furaha sana katika dunia hii, alimpigia mama yake na ndugu zake wa karibu kuwapa taarifa hizo, na baadae wakanza nunua vitu vya mtoto,nguo na vitu vya kuchezea.
Baada ya miezi kadhaa mimi na mume wangu tulienda kwa mganga kuangalia hali ya Mimba tukaambiwa watoto waliopo ni mapacha, na alikuwa ni wa kike na wa kiume.
Cha ajabu siku mbili zilizopita mume wangu aliniamsha usiku wa manane, akaniangalia machoni na kuniuliza.
"Mke wangu nani baba wa hawa watoto wetu?"
Endelea kufuatilia Story kibao zitakuwa zinakuja hapa hapa, kwa maoni na ushauri au unakisa chako tuma kwa barua pepe fredynjeje@live.com au tuwasiliane kwa namba 0654221465 ipo whatsapp pia

No comments:
Post a Comment