Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @officialfredynjejeblog Twitter @Fredynjeje
Meya
mpya wa Manispaa ya KinondoniBoniface Jacob akiwa mbele ya bara hilo
jipya la Manispaa hiyo mapema leo mara baada ya kushinda kwa nafasi ya
Umeya wa Kinondoni kwa kupata kura 38. Kulia kwake ni Naibu Meya,
Jumanne Mbunju (CUF) ambaye pia ni diwani wa Tandale. Kushoto kwa Meya
ni Mkurugezi wa Manispaa hiyo.
Andrew Chale, Modewjiblog
Uchaguzi uliokuwa unasubiriwa kwa hamu kubwa wa kumchagua Meya na Naibu Meya wa Manispaa za Kinondoni na ile ya Ilala ambao umefanyika muda mfupi uliopita umewezesha Umoja wa vyama vinavyounda UKAWA kuweza kushinda kwa kishindo nafasi za Umeya wa Manispa hizo mbili kwa viti vyote.
Kwa upande wa Meya wa Kinondoni, nafasi hiyo imeenda kwa Boniface Jocob (Chadema) ambaye pia ni Diwani wa Ubungo aliyepata kura 38 huku mpinzani wake Benjamin Sitta (CCM) aliyepata kura 20, Kati ya kura 58 zilizopigwa.
Kwa upande wa Naibu Meya nafasi hiyo imechukuliwa na Jumanne Bunju ambaye ni Diwani wa Kata ya Tandale (CUF) ambaye alipata kura 38 huku mpinzani wake Manyama (CCM) kura 19 huku kura moja ikiharibika.
Kwa upande wa Umeya kwa Manispaa ya Ilala imechukuliwa na Charlse Kayoko aliyeweza kunyakua kura 31 huku upande wa CCM Mgombea wake na wajumbe wake wakikimbilia ukumbi na kuambulia kura sifuri (0) na kwa upande wa Naibu Meya ikichukuliwa na Muba Omary (CUF) aliyepata (31) huku naibu aliyegombea naye kutoka CCM akipata kura sifuri (0).
Kwa hali hiyo Ilala na Kinondoni kwa sasa Mameya wake wapo chini ya UKAWA huku uchaguzi mwingine unasubiriwa kwa hamu kubwa ni ule wa Meya wa jiji la Dar es Salaam unaotarajiwa kufanyika baada ya wiki moja.

Wajumbe kamili wa baraza la Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni wakiwa katika sala maalum ya ufunguzi wa kikao cha kwanza cha Manispaa hiyo tangu kufanyika uchaguzi Mkuu Oktoba 2015, kikao hicho kimekaliwa leo 16 Januari katika ukumbi huo Manispaa ya Kinondoni huku kikiongozwa na Meya mpya, Mh. Boniface Jocob.

Kwa mara ya kwanza baraza likiendelea..
CHANZO MO BLOG

No comments:
Post a Comment