Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @officialfredynjejeblog Twitter @Fredynjeje
Asalaam aleykhum! Shoga yangu bila shaka unaelewa kwamba mwaka 2015
uliokuwa na matukio makubwa ya kihistoria duniani na hapa nchini kwetu
kufuatia kuwepo uchaguzi mkuu uliomuwezesha Dk. John Pombe Magufuli
‘Mzee wa kutumbua majipu’ kuingia Ikulu ya Magogoni ndo unaishia.
Ni wazi kwamba unatafakari na kufanya tathmini ya mafanikio
uliyoyapata katika mwaka huu au namna ambavyo hujafanya kitu chochote
cha maendeleo huku ukishuhudia majirani zako wakijenga nyumba, kununua
magari, kusomesha watoto nk.
Tukija upande wa uhusiano, huenda tangu tulipouanza mwaka huu wewe na
mumeo, mpenzio au mchumba wako hamukuwa sawa na matokeo yake ilikuwa ni
migogoro kwa kwenda mbele.
Kama hivyo ndivyo, yakupasa kuwa makini tutakapouanza mwaka mpya wa
2016 kwa sababu hakuna kitu kibaya katika maisha kama migogoro ya
kimapenzi.
Nasema hivyo, kwa sababu migogoro ya mapenzi hukwamisha mambo mengi ya kimaendeleo na kiafya kwani wahusika huwa kwenye msongo wa mawazo unaosababisha afya kuzorota na hata vifo.
Nasema hivyo, kwa sababu migogoro ya mapenzi hukwamisha mambo mengi ya kimaendeleo na kiafya kwani wahusika huwa kwenye msongo wa mawazo unaosababisha afya kuzorota na hata vifo.
Shoga,
kama wewe na mwenza wako hamko sawa naamini mnaelewa kinachosababisha
hali hiyo, kama ni wivu wa kupitiliza, hasira, wizi, uongo, dharau,
uchafu, uchoyo, uvivu ni vyema mkajirekebisha ili muweze kufurahia penzi
lenu.
Kumbuka kwamba, kama kila mmoja wenu hatakuwa tayari kujirekebisha
mkiwa kama mke na mume, wapenzi au wachumba mtashindwa kukutana chumbani
zaidi kwa ajili ya kujiburudisha.
Sasa kama hilo halitafanyika, wewe au huyo mtu wako atakuwa
anazimaliza wapi haja zake kama si kila mmoja wenu kumsaliti mwenzake?
Shoga, kumbuka usaliti ndiyo chanzo cha kuleta maradhi hususan Ukimwi
ndani ya nyumba, hebu boresheni penzi lenu mwaka mpya ili wengine
wawaige naamini itakuwa poa sana. Bye!
Na GPL Tunakaribisha maoni.... usikose keshooo......
No comments:
Post a Comment