Social Icons

Saturday 23 January 2016

WAZIRI KITWANGA: KAMATAMATA INAYOENDELEA KWA RAIA WA KIGENI NCHINI, HAITAGUSA WENYE VIBALI HALALI

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @officialfredynjejeblog Twitter @Fredynjeje

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza na raia wa China wanaoishi nchini, katika sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga alisema Tanzania inatambua ushirikiano mzuri wa miaka mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi nchini, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni, kamwe haitagusa wenye vibali halali. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kaimu Balozi wa China nchini, Zhang Biao akizungumza katika sherehe ya raia wa China wanaoishi nchini ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam, kabla ya kumkaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (hayupo pichani) kuja kuzungumza na mamia ya wachina hao waliohudhuria sherehe hiyo. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga alisema Tanzania inatambua ushirikiano mzuri, wa miaka mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi Tanzania, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni nchini, kamwe haitagusa wenye vibali halali. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto), kwa kutoa hotuba nzuri iliyowafafanulia wachina waishio nchini kuwa Serikali ya Tanzania inawajali na inatambua umuhimu wa ushirikiano wao uliodumu kwa kipindi cha miaka mingi, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi Tanzania, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni nchini, kamwe haitagusa wenye vibali halali. Wachina waishio nchini jana walifanya sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip na kuhudhuriwa na mamia ya wachina hao. Kulia ni Kaimu Balozi wa China nchini, Zhang Biao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Raia wa China wanaoishi nchini wakishindana kula Tunda aina ya Tikiti wakati wa Sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam. Katika Sherehe hiyo ambayo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (hayupo pichani) alikuwa mgeni rasmi ilihudhuria na mamia ya raia hao wa China. Hata hivyo, Waziri Kitwanga alisema raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi Tanzania, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni nchini, kamwe haitagusa wenye vibali halali. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akiwapongeza raia wa China walioshinda mchezo wa bahati nasibu walioucheza katika sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam. Waziri Kitwanga katika hotuba yake alisema nchi yake inatambua ushirikiano mzuri wa miaka mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi nchini, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni, kamwe haitagusa wenye vibali halali. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Kikundi cha Karate kinachoongozwa na raia wa China wanaoishi nchini kikitoa burudani katika sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (hayupo pichani) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo, katika hotuba yake alisema nchi yake inatambua ushirikiano mzuri wa miaka mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi nchini, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni, kamwe haitagusa wenye vibali halali. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Sehemu ya raia wa China wanaoishi nchini, wakimsikiliza kwa makini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba yake kwa Wachina hao katika sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam jana. Waziri Kitwanga katika hotuba yake alisema nchi yake inatambua ushirikiano mzuri wa miaka mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi nchini, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni, kamwe haitagusa wenye vibali halali. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

 KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI,     WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments: