Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje
WATU 239 watatoa ushahidi katika kesi Namba 6 ya 2015 ya kupinga
matokeo yaliyompa ushindi Mbunge wa Jimbo la Vwawa wilayani Mbozi mkoani
Songwe, Japhet Hasunga wa CCM.
Kesi hiyo ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo
kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana kupitia Chadema, Fanuel Mkisi.
Mashahidi hao wataanza kutoa ushahidi Machi 7 mwaka huu. Upande wa
mlalamikaji utakuwa na mashahidi 74 na kwa mshitakiwa ni mashahidi 85
huku upande wa Jamhuri wakiwa 80.
Wakili wa mlalamikaji, Boniface Mwabukusi alidai mbele ya Jaji
Wilfred Dyansobera wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, alisema katika shauri
hilo atawaleta mashahidi 74 kwa ajili ya kutetea hoja za maombi ya
mteja wake.
Wakili Sambwee Shitambala anayemwakilisha mlalamikiwa, Mbunge Hasunga, pia alisema anao mashahidi 85.
Aliomba Mahakama wasitajwe majina yao mahakamani, badala yake watakuwa wakitajwa mara tu wanapohitajika.
Kwa upande wake Wakili Mkuu wa Serikali, Joseph Pande aliiambia
mahakama kuwa upande wa Jamhuri utakuwa na mashahidi 80 ambao watafika
mahakamani hapo kutoa ushahidi wao.
Jaji Dyansobera aliziasa pande zote kuwa mahakama imezingatia kuwa
kesi za uchaguzi zimewekewa muda maalumu wa kuzisikiliza chini ya
kifungu cha 115 cha sheria ya uchaguzi kuwa kesi hizo zinapaswa
kumalizika ndani ya miezi 12.
Chanzo Gazeti la Habari leo
Chanzo Gazeti la Habari leo
No comments:
Post a Comment