Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje
Bondia
Mtanzania Francis Cheka (kulia) akichapana na mpinzani wake bondia
kutoka nchini Serbia, Geard Ajetovic, wakati wa pambano lao la raundi 12
la ubingwa wa Mabara , uzito wa Super Midle wa WBF lililofanyika usiku
wa kuamkia leo kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es
Salaam.
Katika
raundi ya kwanza bondia Cheka alionekana kuanza kwa woga na kumfanya
mpinzani wake kumshambilia kwa ngumi za kushitukiza na kumpeleka chini,
jambo lililomfanya Cheka kuchanganyikiwa na kuhesabiwa na mwamuzi na
kisha kuendelea na pambano.
Baada
ya kwenda chini katika raundi ya kwanza raundi ya pili cheka alionekana
kucheza kwa tahadhari kubwa kwa kupiga na kukimbia huku mpinzani wake
akionekana kujigadi muda wote na kupiga ngumi za kushitukiza zilizokuwa
na madhara kwa Cheka.
Katika pambano hilo Bondia Francs Cheka, aliibuka na ushindi kwa pointi
Cheka akijitahidi kupangua konde la mpinzani wake....
Cheka,
alichanika katika raundi ya nane baada ya mpinzani wake kumbananisha
kwenye kona iliyokuwa na utelezi ambapo aliteleza na kupoteza mwelekeo
na kushambuliwa mfululizo. Na Mafoto Blog.
KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Cheka akijibu mapigo....
pambano likiendelea....
Wakiliana taimingi.....
Mimi sijui hapa Cheka alikuwa akifanya kitu gani sijui alikuwa akikwepa konde ama akijihami kwa kutoka nduki....
Muda wote Mserbia alionekana kujihami kwa staili hii.....
Cheka akitupiamo ......
Hapa sasa hata mimi sijui ilikuwa ni kitu gani kwamba ni konde zito, mieleka ama nini.....
Cheka sijui alikuwa akifanya nini hapa....
Mserbia akitupiamo....
Mwamuzi akimhesabia Cheka baada ya kuanguka katika raundi ya kwanza.....
Cheka akitangazwa mshindi kwa pointi na mwamuzi kutoka chama cha ngumi WBF....
Cheka akishangilia ushindi wake.....
Mashabiki wakimbeba cheka kwa furaha.......
Cheka akivishwa mkanda wa ubingwa.....baada ya kutangazwa mshindi....
Mabondia
wa kike, Lulu Kayage wa Dar es Salaam (kushoto) akichuana na mpinzani
wake Mwanne Haji wa Mbeya, wakati wa pambano lao la utangulizi...Katika
pambano hilo Mwanne aliibuka kidedea kwa pointi.
Sehemu ya mashabiki waliohudhuria mapambano hayo wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea ulingoni...
Mwanne (kulia) akimwadhibu Lulu....
Sehemu ya wanahabari waliokuwepo kuripoti pambano hilo....
Mabondia
Mohamed Matumla (kushoto) na Bakari Mohamed, wakipambana katika moja ya
pambano la utangulizi...katika pambano hilo,Matumla alishinda kwa
pointi.
Cosmas
Cheka (kulia) akichapana na Mustapha Dotto katika pambano lao la
utangulizi, Katika pambano hilo, Cosmas alishinda kwa pointi.
Mwenyekiti
wa Club ya Simba, Godfrey Nyange 'Kaburu' akimvisha mkanda wa ubingwa
wa WBF Cosas Cheka baada ya kumchapa mpinzani wake kwa pointi.
Cosmas akipiga picha na mapromota wake baada ya kutangazwa mshindi...
Dullah
Mbabe wa Dar es Salaam (kulia) akichapana na Bakari Mwakansope, Katika
pambano hili Dullah mbabe, alishinda kwa K/O katika raundi ya Nne.
Mawe yakiendelea.....
Mawe......
Wakiendelea kuchapana....
Mwakansope akipelekwa chini kwa konde zito......
Mwakansope akipata maelekezo kutoka kwa msimamizi wake, Karama Nyilawila........
Pamoja na maelekezo kibao lakini aliporudi tu ulingoni alikutana na konde zito lililompeleka chini kama hivi....
Mwamuzi akimhesabia Mwakansope...
No comments:
Post a Comment