Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje
Rais Mteule Bw. Simon Mwakifwamba .
Na Shamimu Nyaki-Maelezo.
Kufuatia
uchaguzi uliofanyika jana jijini Dar es Salaam wa kutafuta
viongozi wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) viongozi wapya
wamepatikana ambao ni Rais, Makamu wa Rais, pamoja na Wajumbe kumi wa
Bodi watakaongoza Shirikisho hilo kwa kipindi cha miaka minne.
Akisoma
matokeo ya uchaguzi huo, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Filamu Tanzania
Bw. Nico Mathew amesema kuwa, idadi ya wajumbe waliojiandikisha kupiga
kura ilikuwa ni 69 lakini waliopiga kura ni 52 ambapo Bw. Simon
Mwakifwamba aliekuwa anagombea nafasi ya Urais kwa awamu ya pili
alipata kura 47 kati ya 52 zilizopigwa na wanachama wa vyama mbalimbali
vya tasnia hiyo na Makamu wake Bw. Deo Sanga alipata kura 49 kati ya
52.
Wajumbe
wa Bodi waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni Adam Juma Mikidadi, John
Kalaghe, Irene Sanga, Juma Issa, Michael Sangu, Single Mtambalike,
Hussein Athumani, Ummi Mohamed, Nazir Masila pamoja na Alli Mohamed.
Akizungumza
baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo Rais Mteule Bw. Simon Mwakifwamba
ameahidi kuendelea kukuza tasnia ya filamu nchini kutokana na
ushirikiano mzuri uliopo kati ya Serikali na wadau wa Filamu ili kuweza
kuvuka mipaka ya ndani ya nchi kwa manufaa ya wasanii na Taifa.
“Asanteni
sana kwa kuniamini tena kwa awamu nyingine naahidi kufanya kazi kwa
ushirikiano na nyie kwa weledi, ubora na uhitaji ili tufanikiwe
zaidi”, alisema Mwakifwamba.
Ameongeza
kuwa katika awamu hii ya miaka minne ameandaa vipaumbele vitano ambavyo
ni Kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha Sera ya Filamu
inapatikana, kupata elimu kuhusu tasnia kwa wasanii, kuanzisha mfuko wa
maendeleo ya Filamu, na usambazaji bora wa Filamu hapa nchini ili
wasanii wanufaike na kazi zao.
Uchaguzi
wa shirikisho hilo umefanyika kutokana na viongozi waliokuwepo kumaliza
muda wao kwa mujibu wa Katiba ya Shirikisho hilo ambapo viongozi
waliopatikana wameahidi kuleta mabadiliko chanya katika tasnia ya Filamu
nchini.
No comments:
Post a Comment