Social Icons

Monday, 29 February 2016

TPB YATOA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA SACCOS KIGOMA, NI MPANGO WA KUINUA MITAJI YA WAJASIRIAMALI

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya, (kushoto), akimpatia mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni75 Kaimu mwenyekiti wa Saccos ya Ishimwe Kigoma Bi.Gabriela Hangula wakati wa hafla ya kukabidhi fedha kwa vikudi vya benki za vijijini (VICOBA), mkoani humo,. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma. John Ndungulu,
Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Tanzania, (NEEC), Bi. Beng’ Issa na Afisa Mtendaji Mkuu, (CEO) wa Benki ya Posta Tanzania, Bw. Sabasaba Moshingi.Benki ya Posta imekabidhi jumla ya silingi milioni 175 kwa vikundi hivyo viwili ikiwa ni mpango wa kuwawezesha wananchi kwa kuwakooesha fedha kuinua mitaji yao chini ya udhamini wa baraza hilo.
 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya (kushoto), akimpa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 100 Mwenyekiti wa Saccos ya TWCC Kigoma, Dorothy Takwa. Wa pili kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma John Ndungulu, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Uchumi Tanzania Bi. Beng’ Issa na Afisa Mtendaji wa Benki ya Posta Sabasaba Moshingi akishuhudia makabidhiano hayo.
.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Sabasaba Moshingi akiongea na wana-saccos wa Manispaa ya Kigoma-Ujiji, kabla ya kuwakabidhi kiasi cha fedha Shs milioni 175/=kama mkopo ili kuinua mitaji yao. Kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, John Ndungulu, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi Tanzania, (NEEC), Bi. Beng’ Issa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya
Mkurugenzi wa Idara ya Mikopo wa Benki ya Posta Tanzania, Henry Bwogi akimpa zawadi mmoja wa mwanachama wa Saccos, kulia ni Afisa Uhusiano na Mawasiliano ya Benki Tanzania, Timotheo Mwakifulefule. 

No comments: