Social Icons

Friday, 4 March 2016

Bunduki 34 za kivita na za kiraia zilizokuwa zikimilikiwa na wananchi zasalimishwa kwa jeshi la polisi jijini Arusha

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje

 Kamanda Wa Polisi Mkoani Arusha Liberatus Sabas akionesha moja ya baadhi ya silaha zilizosalimishwa na wamiliki na  nyingine zilizotelekezwa porini.

Bunduki 34 za kivita na za kiraia zilizokuwa zikimilikiwa na wanavijiji wa Tarafa ya Sale Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha ,zimesalimishwa ikiwa ni hatua ya kutii agizo la kamati ya ulinzi na Usalama Mkoani humo, iliyotoa siku saba kwa wananchi wote wanaomiliki silaha kuzisalimisha .

Agizo hilo linafuatia kutokana na mfululizo Wa matukio ya mauaji ya watu katika eneo hilo ambao February 21,2016 pekee watu watatu wa Jamii ya wasonjo waliuwawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosaidikiwa kuwa wafugaji Wa kimasai huko katika kitongoji cha Meje Kijiji cha Kisangiro Wilayani Ngorongoro,Kamanda Wa Polisi Mkoani Arusha Liberatus Sabas amesema baadhi ya silaha zilisalimishwa na wamiliki na  nyingine zilitelekezwa porini.
 Chanzo : Michuzi Media Group

No comments: