Social Icons

Friday 25 March 2016

NAIBU WAZIRI WA AFYA, DK HAMISI KIGWANGALLA ATAJA TOFAUTI KATI YA BANGI NA VIROBA

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje
Naibu Waziri wa Afya, Dk Hamisi Kigwangalla jana alitumia dakika kadhaa kutoa ufafanuzi kwa wabunge kuhusu tofauti iliyopo kati ya dawa za kulevya aina ya bangi na pombe kali za viroba.


Alisema pombe yenye kilevi kilichothibitishwa haiwezi kuathiri afya ya mtumiaji kama ilivyo dawa ya kulevya.

Ufafanuzi huo ulitokana na swali la Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya maswala ya Ukimwi,Mohammed Amour aliyetaka kujua tofauti ya kitaalamu baina ya bangi na kiroba  kutokana  na  jinsi zinavyowatesa watumiaji.

Mbunge huyo wa Bumbwini Unguja alisema kuna kiwango kikubwa cha kilevi kilichopo katika viroba kinachoweza kusababisha athari kwa watumiaji.

Akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo kwenye ofisi ya wakala wa maabara ya mkemia mkuu wa serikali, Dr. Kigwangalla alisema:"Madhara yanatofautina, ya muda mrefu na ya muda mfupi.Utumiaji wa bangi unaathiri  mfumo  wa fahamu kwenye ubongo, lakini pombe iliyopimwa kiasi cha alkoholi haiwezi kukuathiri."

Licha ya majibu hayo,Dr. Kigwangalla aliahidi kufuatilia suala hilo katika mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) ambayo inahusika na vipimo kutokana na udanganyifu unaofanywa  na  baadhi  ya  wafanyabiashara.

"Nitafuatilia kwa kina TFDA nione wanafanyaje, kwa nini viroba vimekuwa vikiuzwa mitaani tofauti na viwango halisi vya alkoholi."Alisema

Awali, Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele alisema wafanyabiashara wa viroba wamekuwa wakitumia ujanja wa kuweka nembo ya asilimia ndogo lakini uhalisia wa kiwango cha alkoholi katika kiroba chenyewe ni kikubwa zaidi.

 “Wanabandika asilimia sita kumbe ni asilimia hata 30 ya alkoholi.”

No comments: