Social Icons

Tuesday 1 March 2016

UNCDF YAWAKUTANISHA WATAALAMU WA FEDHA KUTOKA NCHI MBALIMBALI KUJADILI JINSI YA KULETA MAENDELEO KWA KUTUMIA VYANZO VYA NDANI

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Fedha wa Umoja wa Mataifa (UNDCF), David Jackson, (kulia), akitoa mada kwenye mkutano wa siku mbili wa wataalamu wa fedha na wadau wa maendeleo 62 kutoka nchi mbalimbali Duniani, kwenye hoteli ya Hyaatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, Februari 29, 2016. 
Naibu Mkurugenzi Mtendaji Benki ya TIB, Jaffer Machano, akitoa mada kwenye mkutano wa siku mbili wa Wataalamu wa fedha na wadau wa maendeleo 62 kutoka nchi mbalimbali Duniani, kwenye hoteli ya Hyaatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, Februari 29, 2016.
 Mtoa Mada, Suzane Ngane kutoka Cameroun,  akitoa mada kwenye mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT), Habraham Shemumoyo, kitoa mada kwenye mkutano wa siku mbili wa Wataalamu wa fedha na wadau wa maendeleo 62 kutoka nchi mbalimbali Duniani uliofanyika jijini Dar es Salaam, Februari 29, 2016.

Na Beda msimbe
Wataalamu  wa fedha na wadau wa maendeleo 62 kutoka nchi mbalimbali duniani wameanza mkutano wa siku mbili jijini Dare s Salaam kuangalia namna ya  kuwezesha fedha za kusaidia maendeleo endelevu  kwa kutumia vyanzo vya ndani.

Mkutano huo wa siku mbili ulioanza jana katika hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro umelenga kuja na maelezo muafaka ya namna ya kupata fedha za kuendesha na kujenga miundombinu mbalimbali kwa ajili ya miji inayotanuka.

Katika mahojiano na mwandishi wa Mo Blog kuhusu mkutano huo , mmoja wa wakurugenzi wa UNCDF kutoka makao makuu anayeshughulikia uendelezi wa fedha, David Jackson alisema kwamba wataalamu walioalikwa wanatarajiwa kutoka na msimamo unahusu uwezeshaji wa fedha wa ndani.

Alisema wakati dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa ya wananchi kutoka vijijini kwenda mijini uwezo wa majiji mengi duniani ikiwamo manispaa ni mdogo kuwezesha kutengeneza miundombinu na pia kuwezesha ajira.

Alisema  kwa sasa kutokana na uwingi wa watu wanaofurika katika miji, halmashauri  na uhaba wa fedha kutoka katika vyanzo vya mapato kumesababisha kushindwa kuendelezwa mifumo endelevu ya miundombinu na ajira na kulazimisha wataalamu kuanza kuangalia namna nyingine ya kupata fedha.

Alisema mpango wa kutafuta vyanzo vingine vya fedha kwa kuunganisha nguvu nje ya mfumo rasmi umewezekana Tanzania hasa kutokana na manispaa kama ya Kibaha kuwezeshwa kupata fedha za miradi mbalimbali na wengine nao watatoa uzoefu wao.

“Zamani ilikuwa rahisi sana kwa manispaa nyingi kutengeneza mipango ya maendeleo, lakini kwa sasa kutokana na uwingi wahamaji vyanzo vya kawaida vimezidiwa na kuonekana haja ya kutafuta vyanzo vingine ili kuwezesha maendeleo na ajira,” alisema Jackson.

Alisema mataifa yanahitaji sasa kuangalia mifumo yao ya kuwezesha maendeleo endelevu kwa kutumia vyanzo vya ndani ambavyo vinawezekana kupatikana.

Aliongeza kuwa miradi mikubwa ya maendeleo haiwezi kufanywa na vyanzo vya zamani na kutolea mfano mradi wa maji wa Abu Dhabi ambao umewezeshwa kwa kutumia vyanzo vya ndani lakini kwa namna ambayo inasaidia mji huo kuwa na maji ya uhakika pamoja na kwamba vyanzo vyake havifai.

Alisema ni matumaini yake kwamba baada ya kusikiliza mada mbalimbali wataalamu hao watakuwa na nafasi ya kutoa tamko la namna bora ya kushirikisha wadau wa maendeleo wa ndani kutengeneza miradi mikubwa ya huduma kwa jamii.

Pia alisema kwamba washiriki katika mkutano huo wa siku 2 ni pamoja na wadau wa maendeleo kutoka Uswisi, Sweden na Denmark wapo pia wataalamu wa masuala ya fedha, miradi kutoka Afrika Kusini, Ethiopia, Benin, Rwanda, Mali, Senegal,Uganda, Msumbiji, india, Bangladesh , Marekani na Tanzania.

Mkutano huo wa mashauriano uliandaliwa na UNCDF ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa azimio la AddisAbaba kuhusu maendeleo endelevu na umuhimu wa kuimarisha uwezo wa kifedha wa manispaa mbalimbali.
Mchumi Daniel Platz kutoka Umoja wa Mataifa akiwasilisha mada kwa wataalamu wa masuala ya fedha na wadau wa maendeleo waliokutana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Fedha wa Umoja wa Mataifa (UNDCF), David Jackson, (kulia), akizungumza kwenye mkutano wa siku mbili wa wataalamu wa fedha na wadau wa maendeleo 62 kutoka nchi mbalimbali Duniani, kwenye hoteli ya Hyaatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, Februari 29, 2016. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Serikali za Mitaa nchini Uganda, John Genda Walala
 Washiriki wa mkutano wa kimataifa wa siku mbili wa wataalamu wa masuala ya fedha na wadau wa maendeleo wakifuatilia mada ikliyorushwa kwa njia ya video na Profesa Paul Smoke kutoka Chuo Kikuu Cha New York, nchini Marekani.
 Mchumi, John Boex, akitoa mada kwenye ufunguzi wa mkutano huo wa siku mbili ulioanza Februari 29, 2016
 Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Serikali za Mitaa nchini Uganda, John Genda Walala, akiongoza mkutano wakati wa asubuhi
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Fedha wa Umoja wa Mataifa (UNDCF), David Jackson, (kushoto), akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa(UNCDF) nchini Tanzania, Peter Malika.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Fedha wa Umoja wa Mataifa (UNDCF), David Jackson, (kulia), akizungumza kwenye mkutano wa siku mbili wa wataalamu wa fedha na wadau wa maendeleo 62 kutoka nchi mbalimbali Duniani, kwenye hoteli ya Hyaatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, Februari 29, 2016. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Serikali za Mitaa nchini Uganda, John Genda Walala
 Baadhi yawashiriki wakifuatilia kwa makini yanayoendelea katika mkutano
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Fedha wa Umoja wa Mataifa (UNDCF), David Jackson, (kulia), akiwa kwennye mahojiano na Mjumbe kutoka nchini Uganda, Naibu Mkurugenzi wa usimamizi wa mikakati na maendeleo ya biashara, jiji la Kampala, Patrick Musoke, pembezonimwa mkutano wa siku mbili wa wa wataalamu wa fedha na wadau wa maendeleo 62 kutoka nchi mbalimbali Duniani, kwenye hoteli ya Hyaatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, Februari 29, 2016
Wajumbe wakibadilishana mawazo.(Picha zote na Khalfan Said na Geofrey Adroph.)

No comments: