Social Icons

Friday, 29 April 2016

MWANAHABARI MTOTO NA MWANAMAZINGIRA WA UN, GETRUDE CLEMENT AWASILI JIJINI MWANZA.

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje


Getrude (Katikati) akiwa na Wazazi wake, Clement Leon (Kushoto) pamoja na Rizik Athman (Kulia).

Alihudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa nchini Marekani uliohusu Mabadiliko ya Tabia nchi (Climate Change) ambapo alihutubia Ƶakiwakilisha kundi la Watoto na Vijana duniani.

Kutoka Kushoto Pichani ni Brightius Titus ambae ni Katibu wa Mtandao wa Watoto na Vijana Mkoani Mwanza MYCN, Katikati ni Getrude mmoja wa Watoto wa Mtandao huo na Kulia ni Shaban Magana ambae ni Mwenyekiti wa MYCN.

"Kitu ambacho nimejifunza ni kupata kujiamini zaidi kwa sababu ule Mkutano ulihudhuriwa na watu wengi, wakiwepo viongozi kutoka zaidi ya nchi 170 wanachama wa Umoja wa Mataifa. Wameniasa kusoma zaidi ili kufikia malengo yangu ambapo nitaendelea kuzungumza na wananchi pamoja na viongozi wao juu ya masuala ya mabadiliko ya tabia nchi ambapo nitakuwa balozi wao". Alisema Getrude.
"Wazazi wawaruhusu watoto wao katika kushiriki shughuli mbalimbali za vikundi ili waweze kujiamini zaidi katika kufikia ndoto zao". Anasema Mtoto Mwanahabari Getrude.
Shabani Njia (Kulia) ambae ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Vijana na Watoto Mkoani Mwanza MYCN akizungumzia mapokezi ya Mwanahabari na Balozi wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa akiwakilisha kundi la Watoto na Vijana Getrude Clement
Clement Leon ambae ni baba mzazi wa Getrude akizungumzia mapokezi ya mwanae katika Uwanja wa ndege Mwanza.
Rizik Athman ambae ni mzazi wa Getrude akizungumzia mapokezi ya mwanae katika Uwanja wa ndege Mwanza ambapo anafurahishwa na hamasa aliyonayo mtoto wake ikiwemo kujiamini katika masuala mbalimbali ikiwemo ya habari.

Ndugu, Jamaa, Marafiki pamoja na Viongozi wa MYCN, mapema wakifurahia jambo wakati wakimsubiria Getrude
Ndugu, Jamaa, Marafiki pamoja na Viongozi wa MYCN wakiwa pamoja na Getrude.
Ndugu, Jamaa, Marafiki pamoja na Viongozi wa MYCN, wakifurahia na Getrude katika picha ya pamoja.

No comments: