Social Icons

Monday, 25 April 2016

PSPF yavuna wanachama Wilaya ya Temeke

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje

Mtangazaji wa kipindi cha wanawake live kulia Bi. Joyce Kiria kushoto akionyesha kitambilisho  chake cha uchangiaji wa hiari kutoka kwa Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa  mfuko wa PSPF Bi. Mwanjaa Sembe kushoto wakati wa mafunzo kwa wajasiriamali yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa  mfuko wa PSPF Bi. Mwanjaa Sembe kushoto akimkabidhi  Mtangazaji wa kipindi cha wanawake live kulia Bi. Joyce Kiria kitambulisho cha uchangiaji wa hiari katika mafunzo kwa  wajasiriamali yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa  mfuko wa PSPF Bi. Mwanjaa Sembe akitoa mada katika mafunzo kwa wajasiriamali yaliyofanyika jijini Dar es Salaamm jana.

Mtangazaji wa kipindi cha wanawake Bi. Joyce Kiria akitoa mada katika mafunzo kwa wajasiriamali yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Picha na Benjamin Sawe

Mfuko wa Pensheni wa PSPF umevuna wanachama wengi waliojiunga na uchangiaji katika mpango wa haiari (PSS) wakati wa mafunzo kwa wajasiriamali yaliyoendeshwa na Mtangazaji wa Kipindi cha wanawake Bi. Joyce Kiria ambapo PSPF walidhamini na kutoa elimu juu ya Mfuko wa PSPF.

Ili kuwafikia wananchi wote Tanzania Mfuko wa Pensheni wa PSPF una uchangiaji katika mpango wa Hiari,katika mpango huu kiwango cha uchangiaji ni kuanzia Shilingi 10,000 na zaidi, hivyo mwanachama atawasilisha michango yake moja kwa moja kupitia akaunti ya Benki au wakala wa malipo wa M-PESA,Tigo-Pesa au Airtel Money. Katika hili mwanachama yupo huru kuwasilisha michango yao, kwa wiki, mwezi au msimu.

Ili kuwa jirani zaidi Mfuko wa Pensheni wa PSPF umeweka mafao katika mpango wa Hiari (PSS) ambapo mwanachama atastahili kulipwa michango pamoja na faida itakayopatikana kutokana na uwekezaji. Faida huwekwa katika akiba ya mwanachama mara  mbili kwa mwaka katika miezi ya Januari na Julai.

Mafao yaliyopo katika mpango wa Hiari  ni ya aina sita , Fao la Elimu, Fao la Ujasiriamali ,Fao la uzeeni, Fao la Kifo, Fao la Ugonjwa /Ulemavu na Fao la Kujitoa 

Pia Mfuko wa Pensheni wa PSPF, na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF, wameingia makubaliano yatakayowezesha wanachama wa PSPF, kupitia mpango wa Uchangiaji wa Hiari yaani PSS, kuanza kupata matibabu kwenye hospitali zote zenye mkataba na  NHIF. Makubaliano hayo yalitiwa saini siku ya Jumatano Novemba 18, 2015, kati ya Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw.Michael C.t.M


Jiunge sasa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF maelezo zaidi yanapatikana katika tovuti yetu ya www.pspf-tz.org   


No comments: