Meneja Utetezi wa Shirika la kimataifa la OXFAM, Eluka Kibona akizungumza neno la utangulizi wakati wa hafla ya maamuzi ya Fomu za Mama Shujaa wa Chakula shindano linaloendeshwa na Shirika la Kimataifa la OXFAM kwa mwaka 2016
Afisa Miradi kutoka Shirika la kimataifa la OXFAM Kefah Mbogela akizungumzia juu ya Shindano la Mama Shujaa wa Chakula, Umiliki wa Ardhi na Changamoto za ardhi na mitaji ili kujiendeleza.
Katikati ni aliyekuwa mshiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa chakula 2014, Ester Kulwa akiwahamasisha wakina mama kushiriki katika Shindano la Mama Shujaa linaloendeshwa na Shirika la Mataifa la OXFAM
Mwigizaji Maarufu wa Bongo Movie, Jacob Stephen Jb ambaye pia ni Balozi wa chakula na kampeni ya Grow iliyo chini ya Shirika la kimataifa la OXFAM (wa kwanza kulia) akizungumzia jinsi shindano la Mama shujaa wa Chakula lilivyoweza kuwasaidia akina mama.
Balozi wa chakula na kampeni ya Grow iliyo chini ya Shirika la kimataifa la OXFAM, Dina Marios ambaye pia ni mtangazaji wa E-FM Radio akisisiza akinamama warejee mikoani kulima
Balozi wa chakula na kampeni ya Grow iliyo chini ya Shirika la kimataifa la OXFAM ambaye pia ni Fashion Blogger, Shamim Mwasha akiwahamasisha akinamama kujikita zaidi katika kilimo kwa kuwa kinalipa.
Baadhi ya waandishi wa habari pamoja na wageni wengine wakiwa katika hafla hiyo ya maamuzi ya Fomu za Mama Shujaa wa Chakula shindano linaloendeshwa na Shirika la Kimataifa la OXFAM kwa mwaka 2016
Zoezi la kupitia fomu elfu tatu (3,000) za Mama Shujaa wa Chakula shindano linaloendeshwa na Shirika la Kimataifa la OXFAM kwa mwaka 2016 likiendelea
Majaji wakipitisha maamuzi kwa fomu za washiriki wa shindano la mama shujaa wa chakula msimu wa tano, 2016 zoezi litakalochukua wiki nzima ili kuwapata washiriki.
Shindano la Mama Shujaa wa Chakula msimu wa tano limeingia
katika hatua ya pili ya kupokea fomu na kuwachuja wakina mama waliotuma maombi
ya ushiriki wao baada ya hatua ya mwanzo ya kugawa fomu hizo kufanyika katika
uzinduzi wa shindano hilo mkoani Mtwara mapema mwaka huu.
Fomu hizo zimepokelewa leo katika kituo cha mazoezi cha Azura
jijini Dar ambapo timu ya majaji kumi kutoka taasisi mbalimbali walizipitia
fomu hizo katika zoezi litakalochukua takribani wiki nzima hadi kukamilika
kwake.
Kwa mujibu wa Afisa Miradi kutoka shirika la kimataifa la
Oxfam, Kefah John, alisema kuwa takribani washiriki 3,000 wametuma maombi yao
kupitia fomu hizo ambapo katika hatua ya kwanza watapatikana washiriki 28 ambao
watachujwa na kubakia washiriki 18 watakaopiga kambi mkoani Monduli, Arusha na
hatimaye kumpata mshindi mmoja.
Wakizungumza na waandishi wa habari, msanii Jacob Stephen JB
na mtangazaji wa EFM, Dina Marios ambao ni mabalozi wa shindano hilo,
waliwahamasisha wakina mama watumie shindano hilo litakalorushwa laivu kupitia
kituo cha televisheni ya ITV ili kujifunza njia mbalimbali za kuboresha
uzalishaji wao ili kukuza kipato cha familia.
No comments:
Post a Comment