Afisa
Mwendeshaji kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Hadji Jamadary akiongea
na wavuvi,Wafanyabiashara ya samaki pamoja na wajasiliamali waliopo
katika soko la Samaki la Feri
Katibu
Kamati ndogo ya Utawala na Biashara Soko la Samaki la Feri Bw. Daudi
Chiwinga akizungumza jambo wakati wa mkutano huo wa Mfuko wa Pensheni wa
PSPF na wadau wake
Afisa
Mwendeshaji Msaidizi kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Nahshon Mshabaa
akigawa fomu za kujiunga n NHIF kwa wadau wake wakati wa mkutano huo wa
kupokea maoni na kuwaelimisha zaidi juu ya bidhaa za mfuko wa pensheni
wa PSPF.
Afisa
Mwendeshaji Msaidizi kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Nahshon Mshabaa
akiwasaidia kujaza fomu wanachama wapya ambao ni wajasiliamali kutoka
soko la Samaki la Feri waliojiunga na Mpango wa hiari wa PSPF
Afisa
Mwendeshaji kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Hadji Jamadary
akiwaonesha wajasiriamali kutoka Soko la Samaki la Feri(Hawapo pichani)
mafao yatolewayo na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF
Baadhi
ya wajasiliamali kutoka soko la Samaki la Feri wakitoa maoni yao na
kuuliza maswali mbalimbali kwa ma afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF
wakati wa Mkutano huo.
Wajasiliamali na wadau wa PSPF wakitazama moja ya kipeperushi ambacho ni cha Mkopo wa viwanja
Mmoja
wa wajasiliamali kutoka Soko la Samaki la Feri akipokea kadi yake ya
Mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS) kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF
bwana Hadji Jamadary
Baadhi
ya ya wajasiliamali kutoka katika Soko la Samaki la Feri wakisikiliza
kwa makini wakati Mfuko wa Pensheni wa PSPF ulipokwenda kuwatembelea kwa
lengo la kupata maoni kwa wadau wake na kuwapa elimu zaidi juu ya mfuko
huo.
(Picha zote na Fredy Njeje)
Mfuko wa Pensheni wa PSPF leo
hii umeanzisha rasmi mpango wa kukutana na wanachama wake na baadhi ya
wajasiriamali jijini ili kupokea maoni
na kuwahamasisha kujiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS) ili kunufaika
na mafao mbalimbali yanayotolewa na mpango huo.
Akizungumza katika mkutano na
wanachama na wajasiriamali kutoka soko la samaki la Feri Jijini Dar, Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa
Pensheni wa PSPF, Hadji Jamadary alisema kuwa mbali na kupokea maoni wanaendelea
kutoa elimu ya juu ya mpango huo wa hiari ambapo mwanachama atakuwa huru
kuchagua muda wa kuchangia kutegemea kipato chake huku kiwango cha chini
kikianzia Shilingi 10,000 ambayo mwanachama anaweza kulipia kupitia benki na
huduma za simu.
Bwana Hadji alisema kuwa mpango
huo wa hiari unakaribisha raia na mtu asiye raia bila kusahau mjasiriamali na
mfanyakazi wa serikali na kuongeza
kuwa mwanachama anayejiunga katika mfuko
huo huweza kupata mafao ya aina sita ambayo ni; Fao la Elimu, Fao la
Ujasiriamali, Fao la Uzeeni, Fao la Kifo, Fao la Ugonjwa/Ulemavu, Fao la
Kujitoa, na Fao la Matibabu.
Akifafanua kuhusu Fao la
Matibabu, Bwana Hadji alisema kuwa kupitia mpango wake wa uchangiaji wa hiari
wanashirikiana na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambapo mwanachama
ataweza kupatiwa huduma bure katika hospitali na maduka ya madawa
yaliyosajiliwa na NHIF kote nchini.
“Mwanachama anaweza kuwasajili
pia wategemezi wake watano na kuendelea kupata mafao yetu bila shida yoyote,”
alisema Hadji.
Wakizungumza kwa nyakati
mbalimbali wajasiriamali hao walionesha kufurahia unafuu wa mfuko huo na
kuwataka PSPF kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili wananchi wengi wajiunge kwa
kuwa hupoteza fedha nyingi ambazo wangeweza kuziokoa kwa kujiunga na mfuko huo.
Aidha Hadji aliwaambia
wanachama hao kuwa PSPF ina mpango wa kuwawezesha wanachama wake na jamii kwa
ujumla kumiliki nyumba zilizopo Dar , Morogoro, Tabora, Mtwara, Shinyanga na
Iringa ambapo wataweza kununua kwa mkopo au malipo ya mara moja pamoja na mikopo ya viwanja vilivyo sehemu mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment