Social Icons

Friday 5 August 2016

HADITHI YA KUSISIMUA: KIUMBE WA USIKU SEHEMU YA 1-7


“Naitwa Joy.. naishi Tandale. Abeeeh! Nina miaka 18,” hiyo ilikuwa ni sauti ya Joy akijibu maswali aliyoulizwa; akiwa katika moja ya vyumba vya gesti maarufu kwa jina la Kuyangatana Guest House na mzee mmoja wa makamo aliyeonekana kuvutiwa na maongezi kwanza kabla ya kufanya ngono.
Joy aliyeonekana hana muda wa kupoteza alianza kumvua nguo yule mzee, alitaka kumalizana na mteja huyo haraka na kurudi tena uchochoroni ambapo wenzake walikuwa wamejipanga kusubiri wateja wengine wa kiume wenye hamu ya kufanya nao mapenzi.
“Kwa nini unafanya biashara hii wakati wewe ni msichana mzuri ambaye hata naweza kukuoa kabisa,” aliuliza yule mzee huku akijitahidi kuhakikisha ile tomasatomasa ya Joy inatoa majibu sahihi ya kusimamisha mlingoti wake ili uvalishwe kinga na kuanza kuchapa kazi.
“Babu mimi sina cha kukujibu, naomba tufanye tulichokijia!” alijibu Joy kwa ukali na kuendelea kuutomasatomasa mlingoti wa babu hadi ulipoitika.
Akahakikisha anauvalisha mpira na kuuingiza korokoroni. hakuwa na haja ya kuzungusha kiuno wala kuvua nguo zake zaidi ya kupandisha kimini chake hadi juu na kumuachia babu wa watu kiwiliwili kiasi cha kumuacha akihema hovyo juu ya kifua chake kibichi.
“Nikubalie nikuoe wewe mtoto mtamu kweli, aaashhhh mmmmhh! ” yalikuwa ni makelele ya mzee wa watu lakini kutokana na uzoefu wa kazi yake wala Joy hakuhangaika kumjibu lolote yule mzee zaidi ya kuhesabu dakika kimoyomoyo akikadiria mzee huyo atadondokea dakika ya ngapi.
Lakini tofauti na wazee wengine na vijana wengi wa siku hizi, wanaomaliza haja zao ndani ya dakika moja tu, mzee huyo alihimili mikiki, hakutegemea kama mzee huyo angedumu dakika tano.

Maskini Joy akaanza kuhisi kufikishwa kileleni na babu, jambo ambalo hakutaka litokee kwa sababu kama angefika, angeshindwa kuendelea na kazi yake vizuri usiku huo na kushindwa kujiingizia kipato, kutokana na uchovu utakaomkuta.
Akakumbuka kuwa wazee kama hao wengi wao hutumia dawa kuwakomesha machangudoa, “Kama kweli ameninywea ‘mngulyati’!” akajiapiza kimyakimya kuwa atasimama na kumdai mzee huyo amlipe hela yake kwa kuwa amemdanganya.
Kadri muda ulivyozidi kwenda ndiyo yule mzee alivyozidi kumkuna Joy. Mara kadhaa akalazimika kuwaza mambo mengi ili mradi hisia zake zisikubaliane na mawazo yake, kidogo akafanikiwa.
Sasa ilikuwa imefika dakika 9 na mzee wa watu alionekana hana dalili yoyote ya kufikia kileleni zaidi ya kelele zake na miguno ambayo Joy alianza kuhisi ni za uwongo.
“Lazima nimfanyie kitu huyu mzee hanijui,” aliwaza Joy lakini kabla ya kufanya hivyo, akawaza jambo la ujanja. Akajifanya naye amepandisha mzuka ile mbaya, akaanza kuimkatikia mzee na kujifanya analalamika balaa.
Mbinu hiyo ikaonekana kufanya kazi, mzee wa watu akaanza kujikunja akatoa macho kama chura ameona kumbikumbi, akapiga kelele huku amemshikilia kiuno Joy na mara akaanguka kama mzigo juu ya kifua cha Joy.
“Mzee amka unipe hela yangu,” mzee wa watu alionekana amelala kama vile anakata roho, wasiwasi ukaanza kumuingia Joy akatoka nje haraka kuwaita walinzi wa gesti ile ambao ni wamasai ili waone yaliyomtokea chumbani kwake.
“kwani ulifanya nini huyu musee,” aliuliza mmasai mmoja akionekana kuogopa zaidi.
Mzee wa watu alionekana hana kauli huku mkia wake ulioganda na mpira uliojaa gundi, ukiwa bado unaning’inia katikati ya miguu yake.
“Wasee wengine wanapresha halafu wanataka utamu ona sasa. Akitufia tumekwisha” alisema mlinzi mwingine.



Kwa akili ya harakaharaka waliamua kuita bajaji ya mmoja wa madereva wa pale kichochoroni ambao nao walikuwa wakiingiza kipato chao kupitia machangudoa wa maeneo hayo kwa kuwasafirisha wateja wa biashara hiyo kutoka sehemu moja hadi nyingine.
“Huu msala unajua!” alizungumza yule dereva kwa hamaki baada ya kuambiwa kinachoendelea kuhusu yule mzee aliyezirai ghafla baada ya kupewa penzi na Joy.
“Wewe kazi yako ni kumtupa tu huyu mzee mtaroni, kwani kuna ugumu?” alisema Joy kwa woga.
“Nipe elfu ishirini,” aliongea yule dereva.
“Jamani punguzapunguza kidogo hapa ndiyo kwanza nilikuwa naanza kazi, kaka angu,” alibembeleza Joy.
“Aah sista hiyo haipungui kabisa, hii kesi,” “Kaka angu, naomba basi upokee hii, nisaidie kama mdogo wako,” alizidi kubembeleza Joy, akatoa shilingi elfu 15 huku chozi likimtoka.
Yule dereva alimuonea huruma lakini alimpa sharti la kwenda naye hadi sehemu yenye mtaro ili kumtupa yule mzee huyo maana yule dereva alikuwa na wasiwasi kama msala utatokea.
Joy na dereva kwa kificho walimbeba yule mzee na kumuweka kwenye siti ya nyuma ya bajaji, wakamkalisha upande wa kutokea, mwenyewe Joy akiwa amemshikilia kiuno ili asidondoke.
Wakakata mitaa na kutafuta sehemu nzuri wamtupe, bahati nzuri maeneo mengi yalikuwa hayana watu kutokana na muda kwenda sana.
Dereva na Joy wakamshusha yule mzee ambaye bado alionekana kulegea vilivyo, wakamtelekeza pembezoni mwa barabara kisha wakageuza na kuondoka.
Wakiwa umbali wa mita kadhaa Joy aligeuka na kutazama kupitia kioo cha nyuma, akashtuka, akajikuta ameshika mikono kichwani.


Huwezi amini yule mzee ambaye muda mchache uliopita alionekana amezirai, alionekana amesimama na kukimbia tena huku akiwa anacheka kwa sauti; “hahaa uroda burebure.”
Ni wazi kuwa Joy alikuwa ameingizwa mjini na yule mzee ambaye alijifanya amezimia baada ya kufanya naye mapenzi, kumbe lengo lake lilikuwa ni kutolipa hela yoyote baada ya huduma ya ngono.
Wakati yule dereva bajaji akiwa akicheka nusura mbavu zivunjike kwa tukio lile, Joy alikuwa amekasirika kiasi cha kutosha, hasira zilimpanda kwa hasara aliyokuwa ameingia; kwanza ametumika mwili wake bure pasipo kupewa chochote, cha pili alikuwa amelipia elfu 15 nzima ya bajaji kwa ajili ya kuutupa mwili wa mtu aliyedhani amezimia kumbe alikuwa ni tapeli.
Kwa huruma yake yule dereva bajaji aliamua kumrudishia shilingi elfu 10 Joy na kuchukua elfu 5 akamrudisha pale kichochoroni kwa machangu wenzake ambao mpaka muda huo wengine walikuwa wameshaenda na wateja zaidi ya mara tatu na kuingiza mkwanja wa kutosha.
Kwa hasira Joy akaagiza kinywaji kikali cha Kiroba vipakiti vitatu na kuvinywa harakaharaka. Vikamshusha hasira na kubust upya mudi yake.
Akasimama na kutega ndoano yake tena kwa mpita njia mmoja, kijana mtanashati aliyeonekana akienda mbele lakini akili yake shingo yake ikigeuka kama bundi akimtazama Joy kwa jinsi alivyoacha nusu na robo ya umbile lake nje.
“Ni mteja mwenye aibu mfuate,” ni sauti iliyokuwa ikizungumza ndani ya Joy, akaitii na kumfuata yule mtu, “kaka twende nikakupe raha,” alisema Joy bila ya aibu;
“Shingi ngapi?” aliuliza yule kaka aliyeonekana mzoefu ila mdhambi wa sirisiri maana aliongea akiwa gizani kweli.
“Elfu 10 kwa showtime, elfu 30 hadi asubuhi na unanishika kokote unapopenda,” alijibu Joy macho yake yakiwa makavu kweli.
“Poa, twende,” alizungumza yule jamaa , Joy akamuongoza kuelekea kwenye ile gesti yake ambayo muda mchache uliopita alikuwa amenusurika kesi ya mauaji.



Aliingia moja kwa moja na mteja wake ndani na kufunga mlango, akapandisha kimini chake hadi usawa wa tumbo na kujilaza kitandani akimsikilizia mteja wake naye asaule. Hakutaka kufanya kosa kama la yule mzee wa mwanzo akadai hela yake mapema na kupewa kama walivyokubaliana.
Yule jamaa alionekana mzoefu wa biashara hiyo na alionekana anahamu kweli na hilo lilionekana wazi kwa jinsi mlingoti wake ulivyosimama. Moyoni Joy alifurahia wateja wa aina ya yule kaka kwa sababu hakuwa wa kupoteza muda kwenye kale kamchezo kwa sababu hata haikupita dakika mbili yule jamaa alikuwa tayari amefika kileleni.
Baada ya kumaliza, yule jamaa alisimama na kupandisha suruali yake aliyoishusha wakati wa kale kamchezo kachafu. Wakati wanavaa masikio ya Joy yalikuwa makini akasikia kishindo cha kitu kwenye sakafu ya kile chumba.
Alipotazama aligundua waleti ikiwa chini ya uvungu wa kile kitanda, akasimama na kuibana kwa mguu huku akimsubiri yule mteja wake aondoke .
Alipoondoka, haraka akaichukua ile waleti na kufungua ndani yake. Ama kweli mlango mmoja ukifunga mwingine unafunguka. Ndani ya ile waleti kulikuwa shilingi laki mbili taslimu.
Akazificha kwenye matiti yake na kutoka nje haraka, ili asije kukutana na yule jamaa akiwa ameshtuka kama amepoteza fedha zake.
Haya ndiyo yalikuwa maisha ya machangudoa wote hapo kijiweni; siku unakosa, siku unapata. siku unadhurumiwa, siku unadhurumu.


Alisimama na kuchukua upande wa khanga na mkoba wake kutoka kwenye kilinge cha ‘babu’(mmiliki wa gesti) na kujifunga vizuri, hiyo ikiwa ni kuhitimisha kazi yake aliyoifuata usiku huo ambayo iliisha mapema kweli kwa sababu wenzake ndiyo kwanza walikuwa wakianza kazi.
Alichukua kila kitu chake na kupanda bajaji, haraka akiondoka eneo hilo kuelekea mtaani kwake, maeneo ya Tandale. Hakika zari lilimdondokea kiasi kwamba fedha ambazo angepaswa kuzipata kwa kuzihangaikia kwa siku tatu au nne alizipata kwa usiku mmoja tu.
Akamshukuru Mungu wake, akashuka salama na kwenda moja kwa moja kuugonga mlango wa chumba chake, lakini kulikuwa kimya. Akafungua busati la mlango wake na kupapasa chini akachukua ufunguo na kuingia ndani akawa amewahi kabla ya shoga yake, Batuli ambaye muda wake wa kurudi ni saa 10 za usiku.
Wote wawili walikuwa wamepanga ndani ya nyumba hiyo kwa kuchangia chumba kimoja, ni marafiki wa tangu utotoni na wote wametokea Dodoma na kukimbilia Dar kwa sababu ya ugumu wa maisha, mwenzake kazi zake ilikuwa ni kuuza baa huku yeye akiuza mwili.
Kabla usingizi haujampitia aliamua kupekua tena ile waleti yake ili atazame vitu vingine vilivyosalia mle ndani, akagundua kitambulisho cha yule mwanaume jina lake likiwa ni Joseph Gabriel. kimeandikwa CRDB Azikiwe Branch Manager yaani meneja wa tawi la Azikiwe benki ya CRDB.
Akakagua tena, akagundua business card ambayo ndani yake kulikuwa na namba zake za simu na mawasiliano mengine. Akahakikisha hamna kitu tena. Akaviweka vile vitu juu ya dressin tebo na kulala.



Akiwa katika usingizi mzito alishtushwa na hodi, alisimama kivivuvivu na kuufungua mlango. Alikuwa ni shoga yake Batuli, aliyeingia akiwa ananuka pombe. Inawezekana ikawa ni ofa za wanaume zake wa baa.
Kitu cha kwanza alichogundua Batuli mara baada ya kuingia mle ndani ilikuwa ni vile vitambulisho  vya Joy kwenye dressin tebo, akavichukua na kuanza kuviangalia na kuguna.
“Joy huyu nani?” aliuliza Batuli na sauti yake ya kilevi huku akikagua ile waleti.
“simjui,” alijibu Joy akiwa bado na usingizi mzito.
“danga nini shosti? tena anaonekana mtu wa ofisini,” alisema Batuli, alikuwa kidogo hawezi kusoma vizuri kutokana na kuishia darasa la tano, laiti angejua angegundua ni mtu wa benki.
“hahaa danga shoga,” alidanganya Joy na kumficha shoga yake.
“Mh lakini siyo vizuri shoga, inabidi mnitambulishe bwana,”aliongea Batuli kiasi cha kumboa Joy aliyekuwa bado anatamani kulala.
“Sasa ilikuwaje mpaka akasahau vitambulisho!” alizidi kuhoji Batuli kiasi cha Joy kuinuka na kumpokonya Batuli vile vitambulisho na kuviweka ndani ya pochi yake, akiazimia kuvichoma moto mara baada ya kuamka maana hakutaka ushahidi wa vile vitu ili asije akagundulika bure kama alimuibia pochi kaka wa watu.
Japo jua lilikuwa tayari limechomoza na hiyo ikionekana kuwa tayari ni saa 3 asubuhi lakini viumbe hawa wawili ndiyo kwanza walikuwa wakikoroma, wakilipiza usingizi wa jana yake ambao waliukeshea, lakini kwa Joy huenda akawa analipiza usingizi aliohifadhi kuanzia siku za nyuma maana jana yake hakukesha kwa bahati aliyoipata.


Mara nyingi huwa ni njaa peke yake ambayo huwaamsha la sivyo wangeweza kulala mpaka jua lizame ndiyo waende makazini kwao.
Wa kwanza kuamka alikuwa ni Joy ambaye alianza kwa kutazama saa yake kwenye simu yake tena kwa jicho moja kama vile alikuwa hataki kuamka. Alishtuka baada ya kugundua ilikuwa ni saa 10 jioni.
Akasimama na kwenda chooni, akaoga na kurudi tena chumbani. Hapo akavaa dela lake na kutoka nje akielekea kwenye kibanda cha M-pesa maana alikumbuka alipaswa kutuma hela kijijini kwa ajili ya matumizi ya mtoto wake mdogo aliyemuacha kwa mama yake.
Aliingiza hela yote kwenye simu na kutuma shilingi elfu hamsini, akahakikisha tayari imefika kisha akaelekea baa kununua chipsi kuku na kuzila hapohapo baa kichoyo maana hakutaka rafiki yake Batuli amuombe.
Hiyo ilitokana pia na vita baridi waliokuwa nayo wawili hawa; Batuli hakutaka kujiuza, kila siku alikuwa akimshauri rafiki yake aachane na biashara hiyo, wakati huohuo Joy naye alikuwa akimshutumu mwenzake kuwa kazi yake ya baa ina umalaya ndani yake na mbaya zaidi haina hela ya kutosha.
Mara zote ubishi wao huishia kwa kila mmoja kusimamia upande wake.
Lakini ukweli ulibakia palepale kuwa pamoja na kasumba hiyo bado Batuli huwa ndiyo wa kwanza kumuomba Joy hela zake na suala hilo lilikuwa likimuuzi Joy ambaye aliona rafiki yake anamnyonya juhudi zake, si unajua tena kuvumilia purukushani za wanaume ambaye kila mmoja ana ukuni wake, halafu mwenzake anajifanya mlokole baridi, hata mimi nisingekubali kumpa chochote.
Kwa kisasi hicho, Joy alikula chipsi zake na kurudi chumbani,  akamkuta bado mwenzake amelala, akamkagua kwenye pochi yake akaona shilingi elfu 5 tu. Akajichekea kimyakimya na kujisemea kimoyomoyo; “Utakuja tu kujiuza kenge wewe.”

Hakuwa na muda wa kusubiri, ilipofika majira ya saa moja na nusu usiku akaanza kujipara na kuvalia viguo vyake vya mawindoni. Akapendeza sana na ukichangia shepu yake na sura yake nzuri, unaweza kudhani hajazaa kumbe amepitia mambo magumu sana katika maisha yake tena angali akiwa binti mdogo sana.
Mwenyewe akikumbuka haya huishia kumwaga machozi, akajifuta na kujipaka make up kisha juu ya kile kiguo chake akavaa mtandio mwepesi bila kusahau kubeba kanga ambayo siku zote huwa haiachi ndani ya pochi yake.
Akanyanyua simu yake na kumpigia dereva wake wa bajaji. Wakati anamsubiria ndipo kisirani wake akaamka; “nakuona hapo changudoa unaenda kukiuza!” aliropoka Batuli akimtania mwenzake.
“Bora mimi kuliko wewe malaya mkimyakimya unatembea na mizee kwa ofa za bia! utakufa maskini. Halafu hela ya umeme zamu yako wiki hii,” alijibu mashambulizi Joy.
Akasikia bajaji inanguruma nje akachungulia na kugundua ni  bajaji akatoka na kwenda kupanda.
“Joy, kwa hiyo hatuli dada angu!” alisema Batuli kwa unyonge lakini Joy aliondoka kimyakimya kama hajamsikia, akasahau kabisa kuhusu kuchoma vile vitambulisho na business card ya yule mteja wake wa jana aliyempa bingo ya laki mbili.
Akashuka windoni kwake akakiachia kimini chake, akatazama saa yake ya mkononi akagundua ni saa 3 usiku ni muda muafaka kwa ajili ya kazi, Akanunua kiroba kwenye duka la karibu na kujibust nacho ili kukata aibu. Akasimama uchochoroni, akapata mteja wa kwanza, kisha wa pili, lakini wakati anajiandaa kwa ajili ya watatu ghafla akajikuta ameshikwa mkono.
‘Loh ni askari tena wakiwa na defenda, ndani yake wakiwa wamewajaza wenzake kibao, naye  akapakiwa ndani na safari ya kuelekea Oysterbay kituo cha Polisi ikaanza.
Je nini kitamtokea Joy, usikose kesho.

Walipofika kituoni na kuingizwa selo ilikuwa ni kawaida kwa Joy na wenzake ambapo walimalizia masaa machache ya usiku huo na asubuhi ikawa safari ya kuelekea mahakama ya jiji pale Posta karibu kabisa na Kanisa katoliki la St Joseph.
Hapo hutozwa faini ya shilingi elfu hamsini au jela miezi mitatu kwa kosa la uzurulaji na hiyo inatokana na ukweli kwamba sheria ya Tanzania haisemi chochote kuhusu biashara ya ngono hivyo, hata kama polisi watawakamata machangudoa ni lazima wawashtaki kwa kosa la uzurulaji na si vingine.
Hizo ndiyo hatua ambazo Joy akiwa na machangu wenzake walitazamia kuzipitia. Kwa kuwa wengi wao wamezoea kupandishwa mahakamani mara kwa mara na kutoa faini hiyo ya shilingi elfu hamsini, waliona ni jambo jepesi kwao na kuhakikisha hakuna changudoa mwenzao ambaye atakwenda jela, machangudoa kwenye kijiwe cha Joy walikuwa na mfuko wa kusaidiana yaani kama vile vicoba ambapo kila mmoja huchangia shilingi elfu tano kwa wiki ili iwasaidie kwenye masuala kama hayo.
Yaani hata kama changu mwenzao amefiwa hao ndiyo humchangia shughuli nzima za mazishi, sasa vuta picha msiba umedhaminiwa na machangu!
Walikaa ndani ya selo ya mahaka wakiwa na wafungwa wengine wa kike toka sehemu mbalimbali, wakitarajia kesi yao itasikilizwa mapema saa 2 kamili ili saa 4 waondoke hapo mahakamani, lakini tofauti na walivyotarajia hadi majira ya saa 6 asubuhi, hakukuwa na dalili yoyote ya kesi yao kusomwa.
Ilipofika saa 8 mchana walisikia afande mmoja wa magereza akizungumza na wenzake; “Sasa kama hakimu hajaja na hawa machangu si nao tuwapeleke Keko, wakalale hadi kesho?”
“Nini tunapelekwa jela?” aliropoka Suzy akiangua kilio. Kama ulikuwa haujui Suzy mmoja wa machangu wakubwa kijiweni kwa akina Joy na alikuwa mke wa mtu. Hivyo kwa vyovyote hofu aliyokuwa nayo yeye ilimzidi kila mtu hapo ndani maana kama mumewe akimtafuta na kugundua kumbe aliwekwa ndani kwa kujiuza itakuwaje!

Kila mmoja alikuwa na hofu yake kwa wakati huo, si unajua tena wengine walikuwa wanafunzi wa chuo, wengine ndiyo kama Suzy.
Kwa Joy hofu yake kuu ilikuwa ni kwa rafiki yake Batuli ambaye kama akigundua amekamatwa, ndiyo atapata neno la kuzungumza kuthibitisha kazi yake ya baa ni bora kuliko kujiuza, na Joy hakutaka hilo litokee.
Akatulia tuli, kiasi kwamba hata aliposimamishwa na kupakiwa ndani ya basi la magereza, akakaa zake siti ya nyuma akitafakari.
Katika maisha yake hiyo ikiwa ni safari ya kwanza kupelekwa jela, japo kuwa alishawahi kulazwa kituo cha polisi mara nyingi sana.
Mara nyingine humalizana na polisi wanaowakamata hukohuko vijiweni mwao aidha kwa kuwapa penzi au kiasi cha pesa. Tena walifikia hatua ya kujuana na maaskari wengi sana wa vituo vya polisi, lakini mpaka kufikia wanakamatwa basi huenda ni oparesheni maalumu ya Kanda na siyo amri ya maOCD wa vituo vya polisi vidogo.
Walishinda jela siku hiyo nzima na hadi siku ya pili, wakapelekwa tena mahakamani, muda huu kesi yao ilisikilizwa mapema na wakalipa faini na kuruhusiwa kuondoka. Kila mmoja akimlaani hakimu wa mahakama wa jana yake kwa kushindwa kufika mahakamani.
Akiwa anafikiria uongo wa kumpelekea rafiki yake Batuli, akashtukia anaitwa alipogeuka alishangaa kumuona Batuli, lakini kilichomfanya kidogo azimie kwa presha, ni mtu aliyeongozana na Batuli, si mwingine bali ni yule mteja wake aliyemzima zile laki mbili siku mbili zilizopita kule, gesti huku akiviziua vitambulisho vyake nyumbani kwao.

“Shoga pole sana, nini kimekukuta? umenipa wasiwasi kweli yaani,” alizungumza Batuli na kumkumbatia mwenzake, kama vile marafiki wakike wafanyavyo pindi wanapomisiana kwa muda mrefu.
Joy akatumia muda huo kumnong’oneza mwenzake amueleze nini kinachoendelea kati yake na yule kaka aliyongozana naye.
“Niliona kimya nikajua upo naye sehemu. Basi nikampigia simu kutumia zile namba kwenye ile kadi nikashangaa kusikia na yeye mwenyewe akasema anakutafuta kweli, ndiyo tumekuja na nilijua kama sijakukuta hapa jiji basi niende kuulizia mochwari,” alinong’ona Batuli.
Kwa jibu hilo Joy alijikuta akiishiwa nguvu akafikiria kuwa ni bora angemueleza ukweli mwenzake haya yasingetokea, lakini kwa kuwa alimficha basi hayo yalikuwa ni majuto na hana budi kuyapokea.
Akamuachia Batuli na kumfuata yule kaka aliyesimama pembeni, wakati huo akitunga uongo harakaharaka kichwani; “Mambo? Unaitwa nani vile? “ aliuliza yule jamaa huku akimtazama vizuri Joy kama vile alikuwa akiinakili sura yake ili asiisahau.
“Naitwa Joy, najua umefuata waleti yako na kweli nilitaka kukupigia sema ndiyo haya matatizo yamenikuta,” alijitetea.
“Usijali, nafahamu ugumu wa kazi yako, mimi sitaki chochote zaidi ya kile kitambulisho, ile hela unaweza ukakaa nayo tu.”
“waooh kweli?” alijikuta akishangaa Joy kwa sababu wanaume wa Kiswahili hapo ndiyo wangemuanzishia kipigo kikali na matusi huku wakitaka kila mtu ajue kuwa anamdai, lakini tofauti na yule kaka kwani alikuwa mstaarabu sana.
“Yah twendeni, nimekuja na gari,” alizungumza yule kaka akiongozana nao kutoka nje ya eneo la mahakama.
Wakapanda gari ya yule kaka na Joy akawa anaelekeza njia hadi wakafika eneo la Tandale Yemen na kupandisha mtaa wa juu hadi maeneo ya Mafioso kisha hapo wakapaki na safari ya kuelekea mabondeni mtaa wa Bitikilembwe ukaanza.
Itaendelea Jumatatu sehemu ya nane hii si ya kukosa , nimewapitisha kwa ambao mlikosa uhondo wa nyuma

No comments: