Mtaalam
mmoja kutoka Wizara ya Kilimo ameeleza kuwa watu kuogopa kula mboga
mboga ambazo zinamwagiliwa na kwa kinyesi cha binadamu kutoka katika
chemba mbalimbali za maji taka hazina madhara kwa afya ya mwanadamu
isipokuwa watu huona kinyaa na kuhofia kupata maradhi.
Alisema
kwamba kinyesi hicho pamoja na uchafu mwengine unaotoka kupitia chemba
za vyooni huwa na virutubisho na kuongeza kuwa tatizo ni pale
wanaposhuhudia umwagiliaji huo na kuona kwa macho yao , na kupata harufu
mbaya inayotoka katika maeneo hayo.
Aliongeza kuwa athari anaweza akapata yule anayehudumia mbogamboga hizo kwa kuwa yeye ndiye anayeshika uchafu huo moja kwa moja pindi anapo mwagilizia na pia anapolima.
Aliongeza kuwa athari anaweza akapata yule anayehudumia mbogamboga hizo kwa kuwa yeye ndiye anayeshika uchafu huo moja kwa moja pindi anapo mwagilizia na pia anapolima.
Hapa
ni Sinza nyuma ya Shekilango na huu ni moja ya mtaro unaopitisha maji
taka kutoka katika nyumba zilizopo katika eneo hilo na kutumika kwa
ajili ya kumwagilia mboga mboga ambazo mwisho wa siku tunazikuta Gengeni
na kutumia majumbani.
Huu ni Mchicha ambao bado unakuwa kutokana na maji hayo
Mchicha ukiwa unaendelea vizuri kabisa hii ni kutokana na kupata maji hayo yanayotoka katika chemba hizo
Huu ni Mchicha ambao unakaribia kuchumwa na kupelekwa Gengeni kwa ajili ya matumizi ya Majumbani mwetu
Bustani zikiwa katika maandalizi
Kijana
huyu ni mmoja wa wamiliki wa Bustani hizo zilizopo nyuma ya Kituo cha
mabasi cha Shekilango, hapa akiwa anamwagilizia Mchicha wake bila hata
ya wasi wasi wowote kwa kutumia maji taka ambayo yanatoka katika chemba
za vyoo maji haya yanaonekana yana presha ni kutokana na kwamba
wanatumia mota kuyasukuma.
Picha na Fredy Njeje
Insta: @fredynjejephotography
Twitter @fredynjeje
Insta: @fredynjejephotography
Twitter @fredynjeje
No comments:
Post a Comment