Social Icons

Saturday, 17 September 2016

SIKU YA KUSOMA DUNIANI: ROOM TO READ WAADHIMISHA KWA KUSOMA KATIKA HEMA

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0654221465 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @frednjeje Twitter @Fredynjeje
 Baadhi ya watoto wa Darasa la kwanza wakiwa wanajisomea vitabu wakati Shirika lisilo la Kiserikali la Room to Read wakiwa wanaadhimisha siku yao ya kusoma iliyokwenda kwa jina la Siku ya kusoma katika Hema
 Mkurugenzi Mkazi wa Room to Read Tanzania Peter Mwakambwale (wa tano kulia) akiwa na Ofisa Elimu wa Mkoa wa Dar es salaam Mwalimu Raymond Mapunda (wa nne kushoto) akimwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mh. George Simbachawene pamoja na wadau wengine wakiwa wanawatazama watoto wakijifunza kwa vitendo
 Mkufunzi wa Usomaji kutoka Room to Read Tanzania Veronica Mahenge akitoa utangulizi katika Hema la kusomea ambapo kulikuwa na Maktaba ya mfano wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kusoma Duniani yaliyofanywa na Shirika hilo
 Picha ya Juu ni Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Kilomo Zan Kibinda akiwafundisha wanafunzi kwa vitendo namna ya kutamka matamshi wakati wa maadhimisho hayo.
 Wadau mbalimbali wakendelea kufuatilia wanafunzi hao wa Shule ya Msingi ya Kilomo wakijifunza kwa vitendo.
 Watoto wakiendelea kujisomea
 Mkufunzi wa usomaji kutoka Shirika la Room to Read akitoa maelezo kwa ufupi namna wanavyo fanya kazi za kuwafundisha wanafunzi kusoma  na kuandika katika shule ambazo Shrika hilo linaendesha mradi huo.
 Mwalimu wa Shule ya Msingi Buma Hawa Namalenga akiwafundisha kwa vitendo namna ya kutamka matamshi na kusoma wanafunzi wa shule ya Zinga na Buma wakati wakiadhimisha siku ya Kusoma Vitabu Duniani
 Abdullah Sikuwaad(Aliyevaa Miwani Mbele) Mkurugenzi Mtendaji wa Readit Books Ltd,ambao ni wachapishaji wa vitabu vya kielimu vya watoto akitoa maelezo namna vitabu vyao vimeweza kuongeza idadi ya watoto kujua kusoma na kuandika
 Love Kimambo (wa tatu Kushoto) akitoa maelezo ya kina juu ya vitabu vyao
Sharifa Mpokwa(wa pili kushoto) kutoka Mradi wa Elimu kwa Msichana (GEP) wa Room to Read Tanzania akitoa maelezo namna wanavyofanya kazi zao katika maeneo ambayo wanaendesha Mradi
Banda la Haki Elimu
Mkurugenzi Mkazi wa Room to Read Tanzania Peter Mwakambwale akitoa maelezo kwa ufupi kuhusiana na Shirika hilo, na kuwakaribisha wageni wote katika Sherehe hizo na kisha kumualika Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene kusoma hotuba yake
Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda (katikati), akisoma hutuba kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kusoma Vitabu chini ya Hema Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam
Wadau mbalimbali wakiwa katika Sherehe za Maadhimisho ya Kusoma katika Hema wakifuatilia mambo mbalimbali yanayo endelea
Baadhi ya Shule ambapo Room to Read wanaendesha Mradi wao wa Maktaba pamoja na Kusoma wakichukua zawadi za vyeti ikiwa ni pamoja na sifa ya kutunza vema Maktaba walizokabidhiwa
Sherehe ikiwa inaendelea
Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mbaruku kutoka wilayani Bagamoyo wakiigiza Igizo la Almas na Jitu kwenye maadhimisho hayo.
Muongoza Mdaharo wa siku ya Maadhimisho ya kusoma Duniani yaliyofanywa na Room to Read Bi. Demere Kitunga akitoa utaratibu namna ya mdaharo utakavyo endeshwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu  Haki Elimu John Kalaghe akieleza kwa kirefu baadhi ya takwimu zinazo onesha viwango vya Elimu nchini Tanzania.
Mwalimu Luka Mkonongwa akichangia mada katika mdaharo huo ambapo alisisitiza kuwa Taifa lolote likitaka kuendelea ni lazima liwekeze zaidi katika Elimu, Pia amepongeza Shirika la Room to Read kwa juhudi ambazo wanaendelea kuzifanya na kusisitiza wadau wengine waendelee zaidi kuwekeza katika Elimu ili kuondokana na ujinga
Mwalimu Mapunda akiuliza swali wakati wa Mdaharo huo
Mmoja wa wanafunzi aliyekuwepo katika sherehe hizo akiuliza swali la kwa nini wanawake wanafanya vizuri sana Darasani na kuwashinda wanaume lakini ndio hao wanaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya kutokujua kusoma na kuandika?
Seraphia kutoka Right to Play akichangia mada wakati wa mdaharo huo
Joseph Kweka akichangia jambo wakati wa Mjadara huo
Muwakilishi kutoka Kampuni ya Mawasiliano Vodacom Bw. Mazoea akigusia swala la jinsi wao wanavyoshiriki kuhakikisha wanaondoa swala la ujinga Tanzania
Msanii na Mwanamuziki Maarufu Tanzania Vitalis Maembe akieleza ni jinsi gani sanaa inaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa Elimu na pia Sanaa hiyo hiyo inavyoweza kudidimiza katika elimu, aliongeza kuwa ifike wakati wasanii watambue nafasi ya wao kuwakomboa wengi katika elimu kupitia sanaa zao.
Wakiendelea kufuatilia mkutano
Dkt. Kitila Mkumbo kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam akichangia Mada wakati wa Mdaharo huo
Mmoja wa waliofika katika Sherehe hizo akiendelea kuchangia mada
Mwenyekiti wa Chama cha wenye ulemavu Tanzania John Paul akieleza namna ambavyo walemavu wamenyimwa kipaumbele katika swala zima la Elimu na kuiomba Serikali kuwatazama na wao kwani wanahitaji elimu Bora pia.
Mmoja wa Mashuhuda akielezea namna Shirika la Room to Read lilivyoweza kuwakomboa wanafunzi kujua kusoma na kuandika katika maeneo ambayo mradi  huo unafanya kazi na pia kuongeza kuwa Maktaba hizo si kuwa tu zimeongeza kiwango cha Elimu mashuleni lakini pia hata watu waishio maeneo hayo wamejijengea utaratibu wa kwenda kujisomea na kuazima vitabu kwa ajili ya kujiendeleza
Mkurugenzi Mkazi wa Room to Read Tanzania Peter Mwakambwale, akifunga rasmi sherehe hizo na kuwashukuru wote ambao waliweza kufika katika Sherehe hizo na shughuli zote na kusema kuwa wao kama Shirika wapo tayari kusaidia shule yoyote ambayo itakuwa na uhitaji wa wao kuwasaidia.

Eneo la Sherehe hiyo Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam
Picha na Fredy Njeje/ Blogs za Mikoa Tanzania


OFISA Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda kwa niaba ya Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) George Simbachawe, amesema serikali itashirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu kuhakikisha kuwa hadi ifikapo mwaka 2030 wawe wamefuta ujinga nchini.

Mapunda ameyasema hayo jijini Dar es Salaam leo wakati akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya usomaji vitabu kwenye hema yanayoadhimishwa duniani kote. 
Alisema moja ya shabaha iliyopo kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kuhakikisha kila mtoto nchini anapata elimu bure kuanzia darasa la kwaza hadi kidato cha nne.
"Nafahamu shirika lenu la Room to Read limekuwa likitumia mbinu mbalimbali katika kuendeleza elimu bora kwa kuweza kujenga maabara katika shule zetu, kutoa vitabu na mambo mbalimballi katika kupambana na elimu," alisema.
Alisema takwimu za kitaifa za sensa ya makazi na watu katika mwaka 2012 zinaoonesha kuwa asilimia  22 ya watanzania hawezi kusoma na kuandika kwa ufasa, 81.7 ni wenye ya msingi 14.4 ndio wenye elimu ya sekondari na asiimia 2.3 elimu ya  chuo. 
Alisema kiwango hicho kidogo kinasababisha watoto kutokuwa na msingi imara katika kipindi cha mwazoanapoanza shule.
"Kwa mfumo unaofanywa na Room to Read katika kuhakisha wanafunzi wanajua kusomma na kuandika afikapo darasa la tatu ni wazi kuwa serikali tunapaswa kujifunza ili kuhakisha hadi ifikapo 2030 tunakuwa tumefanikiwa kufuta ujinga," alisema Mapunda.
Alisema kaulimbiu ya mwaka huu ya maadhimisho hayo inayosema 'Kuandika yaliyoita, Kusoma yajayo' itumike kutafakari kufuta ujinga.
Awali Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Room to Read, Peter Mwakabwale alisema siku ya usomaji duniani ni siku muhimu kwa wadau wa elimu wakiwemo wanafunzi wenyewe, wazazi, walimu, mashirika yasio ya kiserikali na serikali.
Alisema siku hiyo huadhimishwa kila mwaka  ifakapo Sepemba 9, ikiwa ni kutimiza azimio la Tehrani lilipitishwa mwaka 1965 ambapo kwa mwaka huu wanaadhimisha miaka 50 tangu kuazshwa kwake mwaka 1966.
"Kutokana na kuwepo kwa mitiani ya Taifa ya darasa la saba, sisi Room to Read  na washiriki wezetu tuliona ni vyema kuadhimisha siku hio leo ili kupisha tukio muhimu la wadau wetu," alisema.
Mwakabwale alisema takwimu za Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) za mwaka 2015 zinaonesha hali ya usomaji duniani katika nchi saba Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC), Tanzania ni ya pili kwa kuwa na kiwango kikubwa cha watazania wanaojua kusoma, kuandika na kuhesabu kwa ufasaha kwa asilimia 80.3.
Alisema Nchi ya Burundi inaongoza katika nchi za ukanda huo kwa asilimia 85.6 ya wananchi wake wanajua  kusoma na kuandika kwa kiwango cha juu ukilinganisha na nchi nyingine.
Maadhimisho hayo yalinogeshwa na Taasisi ya Room to Read kwa kufanya maonesho ya vitabu na wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali kupata fursa ya kusoma vitabu na kuulizwa maswali pamoja na kupata zawadi za vitabu

No comments: