Social Icons

Tuesday 27 September 2016

WASOMI TUTUMIE ELIMU YETU KUSAIDIA JAMII YETU- REBECA GYUMI




Na Godfriend Mbuya
Mwanaharakati wa Tanzania wa kupinga ndoa za utotoni,Rebeca Gyumi  ambaye ni Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali, Msichana Initiative linalotetea haki za wasichana kupata elimu amewataka vijana ambao wamepata nafasi ya kusoma kuisaidia jamii katika mambo yanayowakwamisha kimaisha.

Gyumi ambaye  ameshinda tuzo ya umoja wa Mataifa inayotolewa kupitia UNICEF katika kipengele cha mabadiliko ya kijamii ameyasema hayo katika kipindi cha SUPAMIX  alipokuwa akielezea namna ambavyo  ameweza kutambulika na kupewa tuzo na Shirika la UNICEF kupitia Umoja wa Mataifa.

“Hakuna kitu kizuri kwangu  kama kutumia elimu yangu kusaidia jamii ambayo nimelelewa, mimi ni zao la jamii kuona kwamba elimu niliyopata kuna watu walijinyima ili mimi niweze kusoma, ndiyo maana natumia nilichokipata kuweza kurudisha angalau fadhila za jamii yangu” Amesema Gyumi.
Ghumi ameongeza kuwa ni vyema  viongozi ndani ya jamii yetu wakiwafundisha vijana namna ya kuitumikia jamiii yetu kuliko vijana wa kitanzania kufundishwa na mataifa mengine juu ya namna ya kuwa kiongozi bora ndani ya jamiii kwa kuwa jamii ya kitanzania itaendelezwa na watanzania wenyewe .
Kutokana na ujasiri aliouonyesha wa kufungua kesi dhidi ya serikali kuhusu sheria ya ndoa iliyokuwa inatoa fursa kwa mabinti wadogo kuolewa ndipo UNICEF ikaweza kumtunuku tuzo ya kutambua mchango wake, shughuli ambayo ilifanyika nchini Marekani.

No comments: