Social Icons

Friday, 11 November 2016

EATV YATANGAZA MAKUNDI YATAKAYOWANIA TUZO 2016,ZOEZI LA KUPIGA KURA KUANZA RASMI LEO USIKU

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo au Habari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejephotography Twitter @Fredynjeje
 Meneja masoko wa Kituo cha televisheni cha EATV, Roy Mbowe akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, wakati wa kutangaza makundi mapya matatu pamoja na yaliyopita yatakayoshindaniwa katika tuzo za Eatv (EatvAwards) zinazotaraji kufanyika Desemba 10 mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa nchini (BASATA), Godfrey amesema kuwa tuzo hizo zimefata vigezo vyote kwa kuwa wasanii wote ambao wameshiriki katika tuzo hizo wamesajiliwa na basata hivyo wale wote waliojipendekeza lakini awakusajiliwa walikuwa wanajiondoa wenyewe kwenye mashindano kwa kukosa sifa.
 Mwakilishi kutoka Vodacom ambao ni wadhamini wa Tuzo hizo akitaja moja ya Makundi ambao watashiriki katika kinyang'anyiro hicho, na kueleza kuwa Vodacom itaendelea kusapoti sanaa

 Wanahabari wakiwa katika Mkutano huo
 Mwakilishi wa Coca  Cola akishukuru EATV kwa ushirikishwaji wao katika swala zima la Sanaa na kuahidi kuwa wataendelea kusapoti
 Mwakilishi kutoka Benki ya  Barclays  ambao ni wadhamini akielezea namna Benki hiyo itakavyo endelea kutoa sapoti katika kutoa tuzo.
 Mwakilishi wa African Songs wauzaji wa muziki mtandaoni akielezea jinsi watakavyo wakuza wasanii zaidi kupitia tuzo hizo
 Mwakilishi kutoka Innovex akieleza namna watakavyo simamia mchakato wote kuhakikisha haki inatendeka kwa kuhakiki matokeo
 Mwakilishi kutoka Selcom akieleza kwa kina namna watakavyo simamia zoezi la upigaji kura ambalo litaanza rasmi leo usiku
Mmoja wa wanahabari akiuliza swali wakati wa mkutano  huo 
Wanahabari wakiendelea kupata tukio hilo
Picha zote na Fredy Njeje
Insta @fredynjejephotography


No comments: