Social Icons

Thursday 10 November 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AONGOZA WANANCHI WA MKOA WA DAR ES SALAAM KATIKA MAPOKEZI YA MWILI WA SPIKA MSTAAFU MHE. SAMUEL SITTA

Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo au Habari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejephotography Twitter @Fredynjeje

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpokea mjane wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mwandamizi Mstafu Marehemu Samuel Sitta, Mama Margaret Sitta (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Jeneza lenye mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mwandamizi Mstafu Marehemu Samuel Sitta likiwa limebebwa na askari mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwaongoza viongozi mbali mbali wakati wa mapokezi ya mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mwandamizi Mstafu Marehemu Samuel Sitta
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Katibu Mkuu wa UWT Mhe. Amina Makilagi (kushoto) wakimfariji akimfariji Mama Margaret Sitta (katikati) wakati wa mapokezi ya mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mwandamizi Mstafu Marehemu Samuel Sitta kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
...............................................


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameongoza viongozi na wananchi katika mapokezi ya Mwili wa Spika Mstaafu Samuel Sitta katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam ukitokea nchini Ujerumani alipofariki wakati anapatiwa matibabu.

Akizungumzia jinsi anavyomfahamu Samuel Sitta katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema Taifa limeondokewa kiongozi mwadilifu,mzalendo, mchapakazi na mtetezi wa wanyonge hivyo taifa litaendelea kuumuenzi utendaji wake.

Viongozi mbalimbali waliojumuika na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika mapokezi ya mwili wa Spika Mstaafu Samweli Sitta kweye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere ni pamoja na Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Seif Ali Iddi, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika, Kikanda na Kimataifa Dkt Augustine Mahiga na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Baada ya Mwili wa Spika Mstaafu Samuel Sitta kuwasili nchini leo mchana amepelekwa nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam ambapo hapo kesho asubuhi viongozi na wananchi watatoa heshima zao ya mwisho za kuuaga mwili wa marehemu katika viwanja wa Karimjee jijini 
Kwa Hisani ya Michuzi Media Group

No comments: