Jonas Kamaleki, Paris
Tanzania yapongezwa katika Utawala bora kwa kuwa na sheria YA Haki YA kupata Taarifa ambayo utasaidia kupunguza vitendo vya rushwa.
Pongezi hizo zimetolewa leo jijini Paris, Ufaransa wakati wa Mkutano wa Kilele kuhusu Mpango wa Uendeshaji wa Serikali kwa Uwazi (OGP) na Mkurugenzi wa Asasi za Kiraia na Ushirikishwaji wa OGP, Bw. Paul Maassen.
"Haki ya kupata taarifa ni kati ya mihimili muhimu katika kudondokana na vitendo vya rushwa kama ilivyofanya Tanzania na Kenya," alisema Maassen. Amezitaka nchi nyingine ambazo hazijafanya hivyo kuhakikisha zinakuwa na sheria za namna hiyo ili kuongea uwazi katika shughuli za Serikali.
Naye Mtafiti wa masuala ya Habari, Bi Alina Mungiu amesema nchi zilizo na Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa zinafanya vizuri katika kusambaza na rushwa na ufisadi. Amesema hayo wakati akiwasilisha mada kwenye kikao cha Asasi za Kiraia hapa jijini Paris kuhusu ulimwengu wa kidigitali.
Bi Mungiu amesema kuwa Serikali inabidi kufanya shughuli zake kwa uwazi zaidi kwa kutumia Serikali Mtandao (e-government). Aliongeza kuwa Maadili katika jamii ni jambo la kushirikiana baina ya Serikali na wananchi na si suala la Serikali peke yake.
Kwa kufanya hivyo malalamiko ya wananchi kwa viongozi wao yatapungua. " Wananchi wanapaswa kuwa na maamuzi katika mambo yanayowahusu na si kusubiri kuletewa na Serikali," alisisitiza Mungiu.
Mkutano huu wa Kilele umefunguliwa na Rais wa Ufaransa, Francois Hollande na kuhudhuriwa na Viongozi wa nchi zaidi ya 13 akiwemo Rais Barrack Obama na Waziri Mkuu wa Canada ambao wameshriki kwa njia ya video.
Suala la msingi linalojadiliwa ni kuhusu uwazi katika kuendesha shughuli za Serikali ambapo Serikali ya Awamu ya Tano imeonyesha Dhamira ya dhati ya kuendesha shughuli zake kwa uwazi ikiwemo kusambaza na rushwa
No comments:
Post a Comment