Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Mungano wa Visiwa vya
Comoro Mhe. Azali Assoumani walipokutana kwenye ndege katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi
Januari 28, 2017 tayari kwa safari ya Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria
Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU). Rais
Assoumani alikuwa akitokea Comoro kupitia Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu
Hassan atika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar
es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege
kuelekea Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa
Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege
kuelekea Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa
Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wakuu wa vikosi vya
ulinzi na usalama katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 wakati
akielekea kupanda ndege kuelekea Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria
Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Comoro nchini Dk.Ahamada El Badaoui Mohamed
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege
kuelekea Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa
Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wafanyakazi katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo
Jumamosi Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea
Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa
nchi za Umoja wa Afrika (AU).
PICHA NA IKULU
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 28
Januari, 2017 ameondoka nchini na kuelekea Mjini Addis Ababa nchini Ethiopia ambako
atahudhuria mkutano kilele wa 28 wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Umoja
wa Afrika (AU) unaoendelea nchini humo.
Katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Rais
Magufuli ameagwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe.
Kassim Majaliwa na Viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa
Mkoa Bw. Paul Makonda.
Pamoja
na kuhudhuria Mkutano huo, akiwa Addis Ababa Rais Magufuli anatarajiwa kukutana
na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Bara la Afrika wanaohudhuria
Mkutano huo.
Hii
ni ziara ya kwanza ya Mhe. Rais Magufuli nje ya Afrika Mashariki tangu aingie
madaraka kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
tarehe 05 Novemba, 2015
Jaffar
Haniu
Naibu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar
es Salaam
28
Januari, 2017
No comments:
Post a Comment