Jana
jumapili March 26,2017 ilikuwa siku muhimu kwa mwanahabari wa 102.5
Lake Fm Mwanza na mwanablogu wa BMG, George Binagi wa Tarime Mara pamoja
na Miss Upendo Kisaka wa Moshi Kilimanjaro baada ya kuuaga ukapela.
Wapendanao
hao walifunga pingu za maisha katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini
Mwanza na baadaye hafla kufanyika Ukumbi wa Sun City Hotel, Ghana Green
View Jijini Mwanza.
"Ahsanteni nyote mliotusaidia kutimiza ndoto yetu kubwa katika maishani yetu. Familia
yangu, ndugu, jamaa na marafiki zangu. Waumini wote wa Kanisa la EAGT
Lumala Mpya Jijini Mwanza chini ya Mchungaji Daniel Kulola na kila mmoja
kwa nafasi yake, Mungu awabariki.
Mmenionesha upendo wa ajabu mno.
Wazazi
wangu hususani mama mpendwa, nimetimiza deni mliloniachia duniani,
hakika sasa mtapumzika kwa amani, pahali pema, peponi, Amina. Ndoa na iheshimiwe na watu wote, Mungu atuongoze vyema". Mr & Mrs George Binagi.
Shukurani
za pekee pia ziwaendelee best man na best lady, Mr and Mrs, Joel Maduka
kutoka Storm Fm Geita na Maduka Online kwa kufanikisha shughuli hiyo
kwenda vyema.
BMG
inakusihi uendelee kutazama picha za awali za shughuli hiyo wakati
wataalamu wetu wakiendelea kukuandalia picha nyingine ikiwemo picha za
kanisani.


























No comments:
Post a Comment