Mkufunzi
Nuria Mshare akitoa mada kuhusu ushawishi na utetezi kwa maafisa miradi
wa asasi za vijana kuhusu namna ya kufanya shughuli ushawishi, utetezi
na ufuatiliaji wa haki za vijana katika ngazi ya serikali za mitaa,
kitaifa na kimataifa kwenye mkutano uliofanyika jijini Dar es
Salaam.
Saddam
Khalfan (Afisa wa Program - UNA Tanzania) akielezea kuhusu sera ya
maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 na mchakato wa kupitia upya sera hiyo
na mchakato wa kukusanya maoni ya sera ya maendeleo ya vijana kwenye
mkutano uliowakutanisha asasi mbalimbali za vijana kutoka Tanzania Bara
na Visiwani chini ya ufadhili wa The Foundation for Civil Society ili
kuwajengea uwezo katika ushawishi na utetezi na ufuatiliaji wa haki za
Vijana.
Rais
Wa Chama ca Walimu wenye Uziwi(CWUT), Theresia Nkwera(kulia) akipata
ufafanuzi wa mafunzo kwa vitendo kutoka kwa Bi Eliza William wakati wa
uwasilishwaji wa mada kuhusu
usashwishi na utetezi kwa maafisa miradi wa asasi za vijana kuhusu
namna ya kichambua sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 na mchakato
wa kupitia upya sera.
Baadhi ya maafisa miradi wa asasi za vijana wakichangia mada kuhusu sera
ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 kwenye mkutano uliowakutanisha ili
kujadili namna ya kufanya kazi kwa pamoja ili kuwa na sauti moja kwenye
sera ya vijana.
Baadhi ya maafisa miradi wa asasi za vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani wakifuatilia mada kuhusu sera
ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 na mchakato wa kupitia upya sera
hiyo na mchakato wa kukusanya maoni ya sera ya maendeleo ya vijana.
No comments:
Post a Comment