Mratibu wa NES Bw. Benard Baha ambaye pia alikuwa ni muwezeshaji akitoa neno la utangulizi wakati wa warsha ya wadau waliokutana kujadili swala zima la nafasi ya mwanamke katika michakato ya usimamizi wa Ardhi nchini.
Bi
Eluka Kibona Mkuu wa kitengo cha Ushawishi na utetezi kutoka Shirika la
Kimataifa la Oxfam Tanzania, akitoa neno kwa niaba ya Oxfam ambapo
alisema kuwa shirika lao linatetea haki ya ardhi kwa wanawake, aliongeza
kuwa kundi la wanawake wa pembezoni wanayo haki pia ya kumiliki ardhi
na pia ili mwanamke apate haki ya umiliki huo wanatakiwa wawe mstari wa
mbele kutetea,kuwa na maandiko yanayohusu umiliki wa rasilimali
mbalimbali ikiwemo ardhi.
Mgeni
Rasmi Dkt. Adam Nyaruhume Mkuu wa Chuo cha Ardhi Morogoro ambaye pia
alikuwa mwakilishi kutoka Serikalini, aliwapongeza waandaaji kwa
kuanzisha mkutano huo, alisema kwamba katika Wizara ya ardhi
wanalichukulia swala la haki kwa wote sio kwa kina mama tu, kwa wanawake
wanaume kwa kumiliki wa pamoja mali mwanamke pekeyake au mwanaume peke
yake katika sera na sheria zinazotungwa sasa na katika taratibu,
alieleza kuhusu sera ya ardhi. Alisema kuwa tatizo kubwa lililopo ni
kutoka na mizizi ya utamaduni wetu, lakini katika maswala hayo walisha
badilisha taratibu ambayo jamii inaheshimu kwa wanawake na wanaume sawa
hata kwa sera na kwa sheria iliyopo, alisisitiza kuwa elimu itolewe ili
wanawake na wanaume wajue kuwa wao ni wamoja.
Bi. Marygoreth Richard kutoka TALWA akitoa mada juu ya Nafasi ya Mwanamke katika mifumo ya kisheria ya nchi
Baadhi ya wadau kutoka maeneo mbalimbali wakiendelea kufuatilia mjadala huo
Bi.
Josephine Dungumaro(Kulia) Mshauri wa Jinsia kutoka Shirika la
kimataifa la utafiti wa Mifugo(ILRI) akielezea mada juu ya nafasi ya
mwanamke katika maamuzi na umiliki wa ardhi ya jamii/jumuia
Bi.
Rose Royce kutoka Morogoro vijijini akieleza kisa na Mkasa kilichohusu
maswala ya umiliki wa Arhi pamoja na haki ya mwanamke katika
umilikishwaji wa ardhi.
Wadau mbalimbali wakiendelea kufuatilia mkutano huo
Wadau
wakichangia maswala mbalimbali kuhusu nafasi ya mwanamke katika
changamoto ya usimamizi wa ardhi ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya
Mwanamke na Ardhi.
Bi.
Rose George Mbezi ambaye ni Mshosholojia kutoka Wizara ya kilimo
akifafanua na kujibu maswali mbalimbali yahusuyo nafasi ya mwanamke
katika kumiliki ardhi.
Aliyekuwa
Mshiriki wa Mama Shujaa wa Chakula misimu iliyopita, shindano
linaloendeshwa na shirika la Kimataifa la Oxfam Bi. Elisa Simiyoni
akichangia jambo na kusisitiza kuwa elimu hii inayopatikana katika
warsha kama hizo iende iwafikie hata wale wanawake wa kijijini ili
wapate tambua haki zao za kumiliki Ardhi.
Mtafiti kutoka Shirika la TNRF Bi. Anne Manangwa akichangia jambo wakati wa warsha hiyo.
Bi. Amina Ndiko kutoka Shirika la Kimataifa la Oxfam akielezea mambo mbalimbali yanayohusu mwanamke na umilikishwaji wa ardhi
Bw.
Adam Ole Mwarabu akichangia mambo mbalimbali yanayohusiana na mambo ya
nafasi ya mwanamke katika Michakato ya usimamizi wa Ardhi
Bi. Rehema Abdallah (Aliyesimama) akitoa uzoefu wake wa namna alivyo wasaidia wanawake wenzake kuweza kumiliki Ardhi.
Bw.
Joseph Rutaizibwa, Mchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, akitoa mawasilisho ya Serikali kuhusiana na hoja
zilizojadiliwa.
Mratibu
wa Miradi ya Ardhi kutoka Care International Bi. Mary Ndaro akiuliza
maswali mbalimbali ikiwa ni pamoja na bajeti pamoja na maswala ya
wawekezaji hasa katika kumiliki ardhi.
Bi.
Experancie Tibasema Afisa mipango miji Mkuu, Tume ya Taifa ya Mipango
matumizi ya Ardhi, akiongelea mambo mbalimbali ya umilikishwaji wa
ardhi, pia alisisitiza kuwa elimu iwafikie hata watu wa pembezoni ili
wafahamu umuhimu wa kumiliki ardhi.
Mratibu wa Miradi ya Ardhi kutoka Shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania Bi. Naomi Shadrack akiuliza maswali mbalimbali yanayohusiana na nafasi ya mwanamke katika michakato ya usimamizi wa Ardhi.
Mratibu wa Miradi ya Ardhi kutoka Shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania Bi. Naomi Shadrack akiuliza maswali mbalimbali yanayohusiana na nafasi ya mwanamke katika michakato ya usimamizi wa Ardhi.
Bi.
Joina Kisota Lenikamilo kutoka Mvomero Morogoro akitoa mchango wake na
kuomba pia jamii ya wafugaji nao waangaliwe na kupewa miliki za Ardhi
katika maeneo yao.
Warsha ikiendelea
Picha zote na Fredy Njeje/BLogs za Mikoa Tanzania.
No comments:
Post a Comment