Katika
kuendelea na kampeni ya Wanawake na Ardhi wadau mbalimbali wamekutana
jijini Dar es salaam kujadili juu ya 'Nafasi ya Wanawake katika
Michakato ya usimamizi wa ardhi' warsha iliyowahusisha wawakilishi
kutoka Wizara ya Ardhi, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo, Mashirika na
wawakilishi wa wakulima na wafugaji.
Kwa
ujumla warsha hiyo ililenga malengo mbalimbali ikiwa ni pamoja na:
kuelewa michakato ya mabadiliko mbalimbali ya taratibu za usimamizi wa
Ardhi(Mfano marejeo ya sera ya Taifa ya ardhi) na athari chanya au hasi
kwa wanawake wa Tanzania,kusambaza ujumbe wa kampeni ya wanawake na
ardhi kama ulivyokusanywa kutoka kwa wadau ambao ni wakulima wadogo
wanawake,wafugaji na mashirika mbalimbali, pia kupata fursa ya kuipatia
Serikali maoni ya wanawake katika marejeo ya sera ya ardhi ya Taifa.
Bi.
Wiyagi Kisandu kutoka WLAC akitoa mada juu ya uelewa wa maswala ya
kijinsia kwa jamii na wanawake kwa ujumla, ambapo alisema kuwa ni muhimu
Serikali na wadau wengine washirikiane kuwapa elemu ya haki miliki ya
ardhi ili iwe rahisi hata kipindi cha mchakato wa kushughulikia kupata
hati hizo uwe rahisi.
Bi.
Naomi Shardrack Mratibu wa Miradi ya Ardhi kutoka Shirika la Kimataifa
la Oxfam akielezea kuhusu dhana ya kuwawezesha wanawake kumiliki
rasilimali ardhi, pia alielezea utafiti wa maswala ya umiliki wa ardhi
uliofanywa na shirika la Oxfam na namna mifumo dume inavyo wakandamiza
wanawake katika kumiliki Ardhi.
Bw.
Stephano Mpangala kutoka RUDI akielezea kisa mkasa kilichohusu mzee
Kuzenza Magoso(80) ambaye alikuwa na wake sita(6), kwa kutambua umuhimu
wa hati milki ya ardhi aliwapatia wake zake wote hati za kumiliki ardhi
ili kuondoa migogoro ambayo ingeweza kujitokeza mbeleni.
Bi.Elisa
Simioni Aliyewahi kushiriki shindano la Mama wa chakula
linaloendeshwa na Shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania akieleza kisa
mkasa cha namna akina amama walivyoweza kushiriki kikamilifu katika
kupigania na kurejesha msitu kijijini kwao ambao ulivamiwa na kutumika
vibaya
Bw.
Adam Ole Mwarabu akielezea zaidi juu ya Kisa mkasa alichozungumzia Bi.
Elisa Simion kuhusu uharibifu wa misitu na kusisitiza kuwa licha ya
akina mama hao kupigania msitu isiharibiwe, lakini pia akina mama
takribani 100 walikwenda kulala katika msitu huo kwa lengo la kuonesha
kuwa hawakufurahishwa na uharibifu huo, na mpaka sasa hakuna tena
wavamizi katika eneo hilo.
Bi.
Rehema Abdallah mhamasishaji wa umiliki wa ardhi kwa wanawake, alisema
kuwa wao wapo tayari katika kushiriki kuchangia gharama za mchakato wa
kuhakikisha wanapata hati miliki za ardhi kwa kuwa ni kitu cha muhimu.
Mh.
Yannick Ndoinyo Diwani wa kata ya Ololosokwani- Longido akielezea
namna wakina mama walivyopewa nafasi kubwa katika kumiliki ardhi.
Dr.
Adam Nyaruhume Mkuu wa Chuo cha Ardhi Morogoro, alieleza kuwa ni muhimu
kuwajulisha na kuwaelimisha wanakijiji hasa kuhusiana na maswala ya
mipango na matumizi ya ardhi pamoja na umilikishwaji wa ardhi, pia
aliwapongeza Asasi ya RUDI kwa kufanya vizuri katika mipango na matumizi
ya ardhi katika maeneo mbalimbali wanayoyashughulikia.
Bw.
Joseph Rutaizibwa, Mchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya makazi akitoa ushauri kuwa Baraza la Taifa la Uwekezaji
Wananchi kiuchumi lishirikishwe katika michakato hii muhimu inayohusu
maswala ya ardhi.
Bi. Eva Mageni akielezea changamoto mbalimbali ambazo wanakutana nazo wanawake hasa katika umilikishwaji wa ardhi.
Bi.
Rosada Msoma Afisa Maliasili Mkuu kutoka Wizara ya Maliasili na
Utalii,alisema kuwa Wizara inatoa ushirikiano wa karibu kwa wananchi
katika kuhakikisha kuna utunzaji bora wa maliasilizetu.
Wawakilishi
mbalimbali kutoka Wizara ya Ardhi,Wizara ya Kilimo,Wizara ya Mifugo,
Wawakilishi wa wakulima na wafugaji, Asasi za Kiraia za Nchini pamoja na
za kimataifa,na wadau wengine wakiwa katika makundi mbalimbali kujadili
mipango mikakati ya kuendeleza haki za wanawake katika rasilimali ardhi
nchini
Bi.
Anne Manangwa Mtafiti kutoka TNRF akitoa mapendekezo kwa niaba ya Asasi
za Kiraia ambapo kati ya mambo waliyo omba yafanyiwe kazi katika
kampeni ya wanawake na ardhi ni pamoja na, Elimu itolewe kwa njia ya
vyombo vya habari juu ya kumiliki ardhi, haki za wanawake katika
kumiliki ardhi pamoja na ushirikishwaji wa wanawake katika kuandaa
Sera,uandaaji wa mikakati pamoja na kutunga Sheria.
Bi.
Marcelina Kibena Mwakilishi kutoka MVIWATA, wao katika kikundi chao
walitoa maoni kuhusu kutambua makundi mbalimbali kupitia elimu itasaidia
kuondoa mfumo dume,kuhamasisha wanawake katika kushika nyadhifa
mbalimbali za maamuzi, vyombo vya habari kuandaa programu mbalimbali za
uelewa kuhusu kumiliki ardhi na mgawanyo wa rasilimali kuanzia ngazi ya
kijiji.
Wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka Wizara ya Ardhi, Wizara ya
Kilimo, Wizara ya Mifugo, Care
International,WLAC,PINGOs,UCRT,FFH,LANDESA,PWC,NES
na ILRI pamoja na waendeshaji wa kampeni hiyo Shirika
la Kimataifa la Oxfam Tanzania pamoja na TALA wakiwa katika warsha hiyo .
No comments:
Post a Comment